HAFLA ya kuapishwa
wenyeviti wateule wa serikali za mitaa wa Halmashauri ya jijini Tanga, imefanyika
leo na kukamilika kwa kiwango kikubwa kwenye Ukumbi wa Shule ya ufudi Tanga, iliyopo kata
ya Mzingani.
Hata hivyo uelewa mdogo miongoni
mwa wajumbe hao wa serikali za mitaa, waliopatikana katika uchaguzi uliofanyika
hivi karibuni umezua changamoto wakati wa zoezi hilo la kula kiapo hivyo italazimu
kurudiwa kwa baadhi yao.
Akitangaza utaratibu wa
kiapo Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Tanga Aziza Lutalla alisisitiza kuwa
kiapo ni kifungo ambacho hakitakiwi kiwe kimefutwafutwa iwe kwa makusudi au kwa
bahati mbaya, kauli hiyo ilizua minong’ono kwa baadhi yao hadi pale alipotangaza kwamba kwa waliokosea kujaza fomu
zao za kiapo itawalazimu kurudia kuzijaza upya kisha zitawekwa sahihi nayeye kwa
utaratibu utakaopangwa.
“Kiapo ni ushahidi wa
kukubaliana na masharti ya utumishi wa Umaa katika nafasi yako na kukiuka ni
kosa la jinai na kuna adhabu yake kwa mujibu wa sheria za nchi... haitakiwi
kiwe kimefutwafutwa, kwahiyo kama kuna mjumbe aliyefanya hivyo awasiliane na
mratibu wa zoezi upewe fomu nyingine,” aliwasisitizia viongozi hao
Baada ya zoezi la
Kuapishwa kwa Wenyeviti 181, wajumbe mchanganyiko 543 na wajumbe 362 wa viti
maalumu, Mstaiki Meya wa Jiji la Tanga, Omari Guledi aliwasisitizia viongozi
hao kuachana na itikadi za vyama vyao lakini wawe wamoja kwa kufanya vikao kwa
mujibu wa taratbu kwa maslahi ya nchi.
Nao wajumbe hao walizungumza na Mwanamke Makini walibainishwa kuwa licha ya zoezi hilo kukamilika lakini lilikuwa na dosari
ambazo hazina budi kufanyiwa kazi kwa wakati mwengine kwavile sasa limeshapita salama.
“Sina hakika kama wajumbe wote
wanajua kusoma na kuandika, kama ulifuatilia kwa makini mwandishi wengine
hawakuwa wakijaza wala kusema yale maneno ya kuapa, sasa kwasababu tuliapishwa
jumla angalau imewabeba," alisema Hussein Abasi mwenyekiti mtaa wa New Hotel kata ya central
No comments:
Post a Comment