Wajumbe
walimteuwa Mugabe kwa kauli moja katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis
Ababa-Ethiopia.
Uteuzi
wa Mugabe kuongoza muungano huo mkubwa ulio na wanachama zaidi ya arubaini, unaelezwa
kuuingiza doa ndani ya AU, kwani Mugabe hana uhusiano mzuri na mataifa ya
Magharibi, hasa baada ya kukaa uongozini tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru
mnamo mwaka wa 80.
Miongoni
mwa masuala katika ajenda ni vita dhidi ya waasi nchini Nigeria wa
kundi la Boko Haram.
No comments:
Post a Comment