Polisi
wamemtaja Said Kouachi na kaka yake Cherif wanaweza kuwa watu hatari na wenye
silaha.
Cherif
Kouachi aliwahi pia na kuhusika na kupeleka wapiganaji wenye msimamo mkali wa
kidini nchini Iraq.
Vyombo
vya Habari vya Ufaransa vimesema mtu wa tatu ambaye amegunduliwa pia kama ni
mshukiwa Hamyd Mourad mwenye umri wa miaka 18 alijisalimisha polisi baada ya
kuona jila lake katika mitandao ya kijamii.
Baadhi
ya rafiki zake walisema katika mitandao hiyo kwamba alikuwa shule wakati
shambulio hilo katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo likitokea,
ambako watu 12 waliuawa.
Uchunguzi
mkali bado unaendelea kuwasaka watu hao wenye silaha.
Awali
jarida hilo lilipandisha hasira kwa waislamu baada ya kuchapisha kibonzo
walichodai kuwa ni Mtume Muhamad SAW.
Watu
wengine watano wameripotiwa kujeruhiwa vibaya.Gazeti
hilo lililo mjini Paris limekuwa likilengwa na wanamgambo wa kiislamu siku za
nyuma.
Tukio
hilo lilitokea mapema asubuhi wakati watu waliokuwa na silaha walipoingia
katika ofisi za gazeti hilo na kuanza kufyatua risasi na kisha wakatoroka
wakitumia gari.
Rais
wa ufaransa Francois Hollande amelaani shambulizi hilo akisema kuwa nchi hiyo
imepatwa na mshangao mkubwa.
Inaarifiwa
washambulizi walisikika kwa sauti ya juu wakisema ''tumelipiza kisasi kw aniaba
ya Mtume Muhammad.'
Rais
Francois Hollande alisema hapana shaka kwamba shambulizi hilo ni la kigaidi
Waandishi
wanne wa jarida hilo la vibonzo, akiwemo mhariri mkuu Stephane Charbonnier
walikuwa miongoni mwa waliouawa pamoja na maafisa wengine wawili.
Vyombo
vya habari vimewataja wachoraji wengine watatu waliouawa wakiwemo, Cabu,
Tignous na Wolinski. Duru zinasema shambulizi hilo lilifanyika wakati wa
mkutano wa kila mwezi wa uhariri wa jarida hilo.
No comments:
Post a Comment