NA EVELYN BALOZI, KOROGWE
UELEWA mdogo kwa baadhi ya wazazi kuhusu umuhimu wa elimu umeelezwa kuwa janga
la kukwamisha jitihada za serikali nchini kuwapatia elimu bora wanachi wake.
Afisa taaluma wa Korogwe Mji Elius
Mavoa aliiarifu Jambo Leo juzi katika mahojiano maalumu juu ya hali ya elimu
katika Halmashauri
ya Wilaya hiyo yenye zaidi ya Shule za Msingi 133 na Shule za Sekondari 25
ambapo shule za Serikali 24 na jumuiya ya wazazi 1.
Inaarifiwa Mkurugenzi wa Korogwe Mji,
Lewis Kalinjuna katika baraza la madiwani mwanzoni mwa juma aliagiza madiwani
wa kata zote kuwaelimisha wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wazingatie masomo
ili kujenga Taifa lenye wataalamu.
Na katika kuhakikisha hilo Mavoa
alisema halmashauri hiyo imemeba jukumu la kuwasomesha zaidi ya wanafunzi 220 wa
Sekondari na Msingi wanao ishi kwenye mazingira magumu.
Kati ya wanafunzi hao
wanaosomeshwa, wa sekondari ni 120 na wa shule za msingi ni zaidi ya 100.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Mji wa Korogwe Anjelus Bendera akifafanua zaidi alisema hatua hiyo imekuja
baada ya Halmashauri kugugundua uwezo mdogo wa familia huchangia ongezeko la utoro
kwa wanafunzi katika shule mbalimbali.
Alisema Halmashauri hiyo imeandaa
mfuko maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao kupitia kitengo cha ukimwi
na daftari la kuandikisha watoto wanao ishi kwenye mazingira magumu na
hatarishi.
No comments:
Post a Comment