Hata hivyo nchi
hiyo imepiga marufuku ndoa hizo, ambapo mtoto wa kike anaruhusiwa kuolewa
anapofikisha umri wa miaka kumi na nane.
Mkoa wa
Shinyanga ulio kaskazini magharibi mwa Tanzania ndio unaotajwa kuongoza kwa
mimba na ndoa za utotoni, ikilinganishwa na mikoa mingine nchini.
Takwimu kutoka
mashirika mbalimbali ikiwemo UNICEF zinaonyesha kuwa, kwa siku, watoto 16
wanapachikwa mimba za utotoni.
Kwa mujibu wa
wataalamu, hali hii imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu na kwa asilimia kubwa
imezorotesha maendeleo ya mtoto wa kike katika eneo hilo.
Ili kumwokoa
mtoto wa kike kutokana na janga hili, kumekuwa na jitihada mbalimbali kutoka
mashirika yasiyo ya kiserikali za kuwaokoa hasa wale ambao tayari
wameshatumbukia katika dimbwi hilo.
Shirika lisilo
la kiserikali la Agape limeweza kuwaokoa wanafunzi wa kike wapatao mia mbili,
wakiwa wamepitia ndoa za utotoni. Wengine tayari wamezalishwa wakiwa na umri
chini ya miaka 13. Hivi sasa wanaanza maisha mapya ya kusoma.
Mmoja wa
watoto waliokolewa akiwa amejitambulisha kwa jina la Pili Omar, ana miaka 14 na
ni mama wa mtoto mmoja. na amekubali kueleza kilichomsibu.
"Niliolewa kwa
sababu wazazi wangu waliniambia sitaendelea kuwa mzigo kwao, hivyo niolewe ili
nianzishe mji wangu."anasema Pili.
Wazazi na
walezi wa watoto hawa wanalaumiwa kwa kuwalazimisha watoto wao kuingia katika
ndoa za utotoni. Licha ya kukithiri kwa ndoa hizo, pia imebainika kwamba
asilimia 99 ya ndoa hizo hazidumu.
Harieth Kulwa ni mmoja wa waathirika wa ndoa
hizi ambaye ndoa yake imevunjika."Nilidhai kuolewa ndio kutatatua matatizo
yangu, kumbe nilijiongezea matatizo. Mwanamume aliyenioa kwanza alikuwa mkubwa
kwangu, pili alikuwa mlevi…" Anabainisha Harieth.
Hata hivyo,
wanaharakati wa haki za binadamu wanaulalamikia mfumo mzima wa kusimamia sheria
kwa kutowachukulia hatua kali za kisheria watu wanaobainika kuwasababishia
mimba watoto, wakidai kuwa ni kutokana na vitendo vya rushwa vilivyogubika
vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment