WAKAZI wa mjii wa Tanga wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kwenda kujisomea katika Chuo Kikuu Huria (OUT) tawi la Tanga ili kujipatia elimu bora itakayo wasaidia kukuza ufanisi wa shughuli zao za kila siku.
Hayo
yamesemwa katika ufunguzi wa mwaka wa masomo 2014 na mkuu wa Mkoa wa Tanga
Luteni mstaafu Chiku Galawa wakati wa hotuba yake ambaye ndiye aliye kuwa
mgeni rasmi katika ufunguzi huo.
Sanjari
na hayo amewataka pia waajiri kuwapa nafasi wafanyakazi wao pindi
wanapo taka kwenda kujisomea kwani kwakufanya hivyo
kutawezesha kuwasaidia kujipatia elimu
endelevu itakayo weza kuwasaidia kwa mambo mbali mbali
Sambamba
na hayo Mkurugenzi chuoni hapo Rahma Muhamedi amewataka
wanachuo wajue kutumia Computer ili kuweza kujisomea masomo
mbali mbali pamoja na kufanya mitihani inayo tolewa kwa njia ya mitandao.
No comments:
Post a Comment