MKURUGENZI
wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, amekanusha uvumi
uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema jana usiku, kuwa Sitti Abbas
Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Urembo la Tanzania (Redd’s
Miss Tanzania 2014).
Uvumi
wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya
Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema
kutokana na vidole vya lawama anavyonyooshewa kiasi cha kukosa amani,
amelazimika kuvua taji ili awe huru.
“Habari
za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno
mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea
nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua
mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanayeona anastahili taji hili apewe ili
niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili
ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.
Akizungumzia
uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama
lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu
kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment