MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Friday 17 October 2014

LEO NDIO LEO NANI MTANI JEMBE


VIINGILIO:
-Viti Bluu na Kijani: Sh 7,000 [Viti 36,693]
-Viti Chungwa: Sh 10,000
-Viti VIP B na C: Sh. 20,000
-Viti VIP A: Sh. 30,000
*Jumla Viti 57,558

*Tiketi Elektroniki zitauzwa M-PESA, CRDB Simbanking na Maduka ya CRDB Fahari Huduma.
*TIKETI HAZITAUZWA UWANJANI SIKU YA MECHI





LEO Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam utarindima kwa Dabi ya Kariakoo wakati Vigogo wa Soka Nchini Tanzania na Watani wa Jadi, Yanga na Simba, watakapovaana katika pambano lao la kwanza la Ligi Kuu Vodacom kwa Msimu wa 2014/15.

Watani hao wanatinga kwenye kimbembe hiki kinachongojewa Nchi nzima hasa kwa vile Msimu huu kila Timu ina Benchi la Ufundi jipya kwa Yanga kuwa na Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania kutoka Brazil Marcio Maximo, na Simba kuongozwa na Kocha wao wa zamani Mzambia Patrick Phiri.

Vile vile mvuto zaidi ni ule wa kuona Wabrazil wa Yanga, Kiungo Andrey Ferreira Coutinho na Geilson Santos ' Jaja' wakivaana na Simba iliyomteka Straika wa Yanga, Mganda Emmanuel Okwi.

Hii itakuwa Mechi ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Yanga wanaingia wakiwa Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 6 wakati Simba wako Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 3.

Msimu huu, Yanga walianza kwa kuchapwa 2-0 na Mtibwa Sugar huko Morogoro na kisha kushinda Mechi mbili mfululizo dhidi ya Ruvu JKT na Prisons, zote kwa Bao 2-1 kila moja.

Simba wao hawajafungwa lakini hawajashinda hata Mechi moja katika Mechi 3 walizocheza kwa kutoka Sare na 2-2 na Coastal Union na Sare za 1-1 dhidi ya Stand United na Polisi Morogoro.

Katika Misimu miwili iliyopita, Matokeo katika Dabi ya Kariakoo ni 1-1 Msimu wa 2012/13 na Yanga kushinda 2-0 Mechi ya Marudiano na Msimu wa 2013/14 kutoka Sare Mechi zote mbili za Bao 3-3 na kisha 1-1.

Hivi sasa kila Timu imejichimbia kwenye Mazoezi makali kwa Simba kukimbilia huko Afrika Kusini na Yanga kubakia Jijini Dar es Salaam wakifanya Mazoezi yao Uwanja wa Boko Veterani.

ONYO KALI: Mashabiki hawaruhusiwi kuingia Uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa
BARABARA: Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.

Refa wa mtanange huu wa ni Israel Nkongo ambae atasaidiwa na Ferdinand Chacha na John Kanyenye wakati Hashim Abdallah atakuwa Refa wa Akiba na Kamishna ni Salum Kikwamba.

Msimu uliopita, Refa Israel Nkongo ndie aliesimamia Mechi ya Mahasimu hawa ambapo Yanga waliongoza 3-0 hadi Mapumziko na Simba kuweza kurudisha na kupata Sare ya 3-3.

MICHUANO MINGINE RATIBA: Jumamosi Oktoba 18
Polisi Moro v Mtibwa Sugar
Ndanda FC v Ruvu Shooting
Kagera Sugar v Stand United
Coastal Union v Mgambo JKT
Mbeya City v Azam FC

No comments:

Post a Comment