WAKRISTU nchini wametakiwa
kuzifanya familia zao kuwa ni chanzo cha upendo, furaha na uimara katika imani ili
kupunguza maovu ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa na Padre
Prochecy Kasongo Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Patriki Jimbo Katoliki la
Morogoro ambaye ni katibu wa tume ya familia wa baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
kwenye adhimisho la ibada ya misa takatifu ya jumapili.
Katika ibada hiyo iliyoadhimisha
kanisa kuu la mtakatifu Anthony wa Padua jimbo la Tanga Kasongo alisema kila
mmoja ndani ya familia anatakiwa kuishi kikamilifu na kujitambua nafasi yake ili
kuwa na maisha ya kumpendeza mungu.
Hata hivyo padre Kasongo hakusita
kuwakumbusha wakrtistu kutambua kila mwanadamu ameubwa kwa makusudi ya Mungu
hivyo basi ni vyema kutambuwa uthamani wapekee machoni pake, kwa tutimize
wajibu wa kumcha yeye muumbaji wetu.
No comments:
Post a Comment