MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Tuesday 14 October 2014

NYAMA ZA KUKU SI TATIZO TENA DAR, PWANI



TATIZO la upatikanaji wa nyama za kuku katika mikoa ya Pwani na Dar es salaam limepatiwa ufumbuzi baada ya Jeshi la kujenga Taifa JKT Ruvu mkoani pwani kuongeza kuzalishaji kutoka kuku wa kisasa 1200 hadi 3000 kwa wiki.


Mbali na mafanikio hayo pia kambi hiyo ya mafunzo ya awali ya kijeshi imefanikiwa kuongeza uzalishaji kuku wa asili 270 hadi kufikia 1700 kwa wiki.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na ofisa wa jeshi hilo Luthen kanali  Charles Mbuge na kuongeza kuwa lengo la kuongeza uzalishaji huo linatokana na kukua kwa soko la nyama za kuku badala ya Ng'ombe na Mbuzi na kuliongezea pato na kukuza uchumi wa jeshi kupitia uzalishaji huo.


"vijana mnajua ajira sio mbaka uajiriwe na serikali au na mtu mkashinda mnapigizana kelele za kukatwa mishahara na kutowajibika bali hata ukiamua kujiajili kupitia kilimo na ufugaji unatoaka kimaisha"asema.

Nae daktari wa mifugo jeshini hapo Jonathani Mgomi alibainisha changamoto wanayakabiriana nazo kuwa ni kuuziwa madawa feki za mifugo kutokana na kukua kwa soko huria jambo linalorudisha nyuma jitihada za jeshi kuondokana na umaskini.

Sanjali na hilo pia alisema ili kuvutia soko tayari jeshi limepunguza bei za malighafi zinazo zalishwajeshini kambini hapo kwa lengo la kuvutia wawekezaji katika sekta ya mifugo na kuwainua wananchi wenye nia ya kufanya kazi hiyo ya ufugaji.

"mfano vyakula vya kuku vimeshuka na kulazimu Trei la mayai ya kisasa kufikia shilingi 6,500 kuku wa kienyeji shilingi 7,000 wakati vifaranga vinauzwa kwa shilingi 1,100 badara ya 1400 na wale wa kienyeji wakiuzwa shilingi 1,200 badala ya 1700"alisema Mgomi.


No comments:

Post a Comment