KAMPUNI ya Angels Moment ya
Jiiji Dar es salaam kuwapatia wanawake wapatao 300 wajasiriamali wa Mkoa wa
Tanga elimu ya biashara katika kampeni ya MWANAMKE NA UCHUMI ili kuwajengea
uwezo na uelewa utakao ibua hisia chanya kutambua fusa walizonazo kiuchumi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yatagusa
masuala ya Ujasiriamali, Utunzaji wa hesabu za Biashara, uwekaji wa Akiba,
umuhimu wa rasimali Ardhi na masuala ya Afya bora.
Akizungumza kwenye mkutano a
waandishi wa habari wa mkoa wa Tanga, Mkurugenzi wa Kampeni ya Wanawake na
Uchumi kutoka kampuni ya Angels Moment, Mahada Erick amesema kuna fursa nyingi
za utajiri kwa wajasiriamali ambazo wengi wameshindwa kuzitambua kutokana na
uelewa mdogo walionao.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Halima Dendego (mwenye nguo ya manjano), pamoja na Mkurugenzi wa Kampeni ya Wanawake na Uchumi kutoka kampuni ya Angels Moment, Mahada Erick. |
"wanawake wengi wakiwemo wa
Mkoa huu wa Tanga, kama mnavyojua wamekuwa wahanga wa kukumbwa na madeni, na
kukatiza biashara na ujasiriamali kwa sababu ya kukosa elimu au kukumbwa na
changamoto mbalimbali,” alisema Erick na kuongeza.
Moja ya changamoto ni
kufanya manunuzi yasiyo yalazima mfano magauni mengi, dhahabu huku wakishindwa
kuelewa kuwa hivyo vitu ni mtaji na vinaweza kununulia mashamba na rasilimali
nyingine za kuendeleza biashara.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga
amesema kuwa semina hiyo itakayofanyika Naivera Complex Novemba 5 na 6 mwaka
2014, imekuja kwa wakati muafaka kwa wajasiriamali kujikuza kibiashara na
kiuchumi.
Kwa upande wao afisa
mwandamizi Uendeshaji kutoka shirika la hifadhi ya jamii NSSF Donald Lembeli na
Baraka Mtoi Afisa Masoko mfuko wa GEPF Mkoa wa Tanga, wamesema kupitia mpango maalumu
wa kuwakomboa wanawake wtakuwa bega kwa bega kuendelea kuwahamasisha ili waweze
kukopesheka fedha za mashirika kupitia kwenye saccos na kujiwekea akiba.
Kwa upande wao afisa
mwandamizi Uendeshaji kutoka shirika la hifadhi ya jamii NSSF Donald Lembeli na
Baraka Mtoi Afisa Masoko mfuko wa GEPF Mkoa wa Tanga, wamesema kupitia mpango maalumu
wa kuwakomboa wanawake wtakuwa bega kwa bega kuendelea kuwahamasisha ili waweze
kukopesheka fedha za mashirika kupitia kwenye saccos na kujiwekea akiba.
Angels Moment wa
kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii jinsia na watoto pamoja na taasisi
ya WAMA imeshanufaisha wanawake 1600.
Kampeni hii pmoja na Mkoa
wa Tanga inatarajia kuwafikia wanawake wa vikundi vya ujasiriamali, SACCOS,
VICOBA na makundi mengine ya kijamii kwenye mikoa ya Pwani, Lindi, Ddodoma,
Kigoma, na Ruvuma.
Waandishi wa Habari wanaume (waliosimama) katika picha ya pamoja. |
Waandishi wa Habari wanawake (waliosimama) nao hawakuwa nyuma. |
No comments:
Post a Comment