Kauli
hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakati wa mkutano wa synodi
ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja wana zawadi na
viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa
mapema wiki hii.
Ripoti
hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya
kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za
wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa
jamii zao.
Na
moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali
ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti.
Zaidi
ya maaskofu 200 wa kanisa katoliki wanakutana kwenye mkutano wa synodi tangu
mapema mwezi huu,katika mkutano huo ni papa Francis aliyetoa mwito wa kujadili
masuala ya utoaji wa mimba,vidonge vya uzazi wa mpango,mapenzi ya jinsia moja
na talaka.
Papa
Francis amewataka viongozi wa juu wa kanisa hilo kuzingatia Zaidi suala la
wapenzi wa jinsia moja chanya kuliko kuwa kinza na amefanikiwa kuwateka
maaskofu wanaohudhuria mkutano huo wa sinodi.
Mwaka
uliopita katika ripoti aliyo itoa papa Francis kuhusiana na mwenendo wa kanisa
katoliki kuwa waumini walio wengi waliliacha mkono kanisa hilo kutokana na
mafunzo yahusianayo na ngono na dawa za uzazi wa mpango.
Papa
huyo anazichukulia ndoa hizo za jinsia moja kama zisizo na utaratibu akiinukuu
ripoti ya kanisa katoliki iliyochapishwa mwaka 1986,wakati Papa Francis
alipokua mshauri mkuu wa masuala ya teolojia ya kanisa katoliki wa hayati papa
John Paul wa pili.
Nguvu
kubwa ya vikundi vya kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja ni juu
ya kauli ya papa Francia aliyoitoa mwishoni mwa mwaka wa jana alipokuwa kwenye
kambi ya vijana wa kanisa hilo huko Rio de Jeneiro alitoa kauli kua kama mtu
anamtafuta Mungu na ana nia njema ,yeye ni nani wa kuhoji?
Papa
Francis anaingia katika historia ya kanisa katoliki ulimwenguni kutumia jina
(hasha kum si matusi) WASENGE hadharani kuliko kutumia neno wapenzi wa jinsia
moja.
No comments:
Post a Comment