WANANCHI Jijini Tanga, wameelezwa
kwamba suluhisho pekee la kuondokana na umasikini ni kujiunga na Mpango wa
Kukopeshana Sedit Vikoba ambao umeonesha watu wengi kujiendeleza kiuchumi
katika familia zao.
Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu
wa kwanza wa vikundi vya Vikoba vilivyopo katika Jiji la Tanga uliofanyika juzi
kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tanga Eckernforde, Mwenyekiti wa shirikisho la
Vikoba nchini George Sweveta, alisema ili watuwaondokane na umasikini ni
kujiunga kwa wingi na mpango huo.
"Ndugu zangu wana-Tanga,
mmechagua mlango sahihi kwa kujiunga na mpango huu wa Vikoba, mkivitumia vizuri
kwa kufuata masharti yake na taratibu zake mnaweza kuwa matajiri kama watu
wengine," alisema Sweveta ambaye kabla ya mkutano huo alivitembelea
vikundi takribani 30 vilivyo Jijini hapa.
Alisema kuwa ili Vikoba katika Jiji
la Tanga viweze kuinuka na wananchi kuondoa umasikini wameandaa mkakati wa
kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wana-kikundi ambao kupata kwao mafunzo hayo
kutawaweka kujua mbinu na taratibui za kuendesha vikoba kisasa na kitaalamu
zaidi.
"Ni vema mkaelewa mbinu za
kupanda na kusimamia mambo ya uchumi...Sababu mnaweza kuweka na kupata fedha
nyingi za mkopo lakini mkashindwa namna bora ya kurejesha mikopo hiyo, lazima
muwe tayari kujifunza kutoka Sedit-Vikoba," alisema.
Alisema shirika la Sedit Vikoba
wameliunda tangu mwaka 2002 katika wilaya ya Kisarawe na Zanzibar ambapo
wadhamini wakubwa ni wanachama wenyewe, serikali na wafadhili mbalimbali
watakaojitokeza kufuatia wanachama kufanya vizuri katika michango yao.
Mwenyekiti wa vikundi vya Sedit-Vikoba
katika Tanga Dkt Ali Buge na katibu wake Elda Kishimbo, aliwata wana-Vikoba
katika Jiji la Tangakwa kushirikiana kuhakikisha lengo la kuondokana na
umasikini linafanikiwa kupitia mpanmgo huo.
Vikoba hivyo wamepanga Novemba 11
kuvizindua rasmi kwa kumwalika kiongozi mkubwa wa serikali katika sherehe
ambayo wanatarajia kwamba itafana kutokana na kwamba vikundi vingi
vitaongezeka.
No comments:
Post a Comment