Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga (TWMO) Bertha Mwambela (wapili kutoka kushoto) na wanachama wa chama hicho kwenye kikao cha maandalizi ya Kufanya usafi, kituo cha afya Pongwe. |
CHAMA cha waandishi wa
Habari Wanawake Mkoani Hapa, Tanga Women in Organization (TWMO) kesho watafanya
usafi katika kituo cha afya Pongwe, tarafa ya Pongwe, kilichopo kwenye
Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Kituo
hicho kilicho chini ya Mganga Mfawidhi, Dk. Faisal Ali, kinapokea mamia ya
wagonjwa kwa siku kutoka vijiji mbalimbali wakiwemo wajawazito na watoto.
Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga wakiwa kwenye kikao chao cha maandalizi ya Kufanya usafi, kituo cha afya Pongwe. |
No comments:
Post a Comment