MSANII 'YP' ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambikile toka kundi la TMK Wanaume Family amefariki dunia Oktoba
20, 2014 majira ya usiku katika hospitali ya Temeke ambako alikuwa akipatiwa
matibabu.
‘YP’ alikuwa akisubiliwa na kifua kwa muda mrefu lakini hali ilikuwa
mbaya katika wiki mbili kabla ya kifo chake.
Kwa mujibu wa Meneja wa TMK Wanaume Family Said Fela
amethibitisha kutokea kwa msiba huo.
Msiba wa msanii huyo uko Keko nyumbani kwa baba yake.
Said Fella amesema Marehemu alifanya vizuri na
msanii mwingine Y Dash na nyimbo kama 'Pumzika', 'Ulipenda Pesa', 'Shemsha' na
nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama 'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka
Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' nk.
No comments:
Post a Comment