Kamanda wa Jeshi la Polisi Tanga, Freser Kashai |
KIJANA mmoja, mkazi
wa Makorora mkoani hapa amepatikana na noti 11 bandia za shilingi elfu 10 za
kitanzania zenye thamani Tshs.110,000 na noti nne za dola 100 bandia za kimarekani
.
Khalid Ramadhani kijana
wa miaka 28 amepatwa na noti hizo Octoba 19, 2014 mnamo majira ya saa 10 za jioni
kwa saa za Afrika mashariki.
Kijana huyo
ameelezwa kuwa ni mkazi wa Mikanjuni kata ya Mabawa Tarafa ya Ngamiani kati
Wilaya ya Tanga mjini Mkoa wa Tanga.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna
mwandamizi Msaidizi wa Polisi, SACP Freser Kashai amesema mtuhumiwa huyo
amekiri kufanya biashara hiyo ya uuzaji wa noti bandia.
Ramadhani atafikishwa
mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma za biashara hiyo haramu baada ya
upelelezi kukamilika.
No comments:
Post a Comment