SERIKALI imeshauriwa
kuendelea kutoa Elimu kwa wanachi wote juu ya umuhimu wa chanjo ya magonjwa ya Surua na Rubella inayo endelea
kutolewa hapa nchini kutokana wananchi wengi
waliojitokeza kuwa na uelewa mdogo kuhusu chanjo hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mwalimu
Asha Mbwana wa shule ya msingi Chuda ambaye niongoni mingoni mwa watoa huduma
kwa wananchi katika hospitali ya Ngamiani jijini Tanga wakati
akizungumza mwandishi wa redio huruma hospitalini
hapo.
Aidha mwalimu huyo amesema
kuwa uelewa wa wananchi juu ya zoezi la chanjo inayotolewa hivi sasa imekuwa ni
ndogo hivyo ameishauri serikali iendelee kutoa ushikiano na cvyombo vya habari
ili kuhakikisha wananchi wote wanaelewa umuhimu wa huduma hiyo.
Naye afisa Afya wa
hospitali ya Ngamiani Alfa Allan Ameishukuru serikali kwa jitihada za
uhamasishaji wa kuhudhuria chanjo kwani wanapokea takribani watoto 500 kwa siku huku watu wazima ni
1000 wanaofika hospitalini hapo.
Sambamba na hayo ametoa
wito kwa wananchi wote kupenda kupima afya zao mara kwa mara ili kujua
maendeleo ya afya zao lakini pia kuwa wakweli pale wanapohisi kuwa na dalli zozote
wa magonjwa ili wqapatiwa matibabu kwa haraka na kwa wakati.
No comments:
Post a Comment