CHAMA
cha waandishi wa Habari Wanawake TMWO Mkoa wa Tanga kimetoa rai kwa wanahabari
wengine kote nchini kujihusisha moja kwa moja kwenye shughuliza kijamii ili
kuweza kugundua changamoto zao kwa njia ya kirafiki.
Waandishi
wengi wa Habari wamekuwa na mazoea ya kuandika habari kwenye matukio maalumu au
kufanya uchunguzi baada ya kupokea ruzuku huku wakisahau kuwa kuna ushirikiano mzuri
unaopatikna kwenye kutoa taarifa kama watajihusisha na wanajamii kuwa sehemu
yao.
Rai hiyo
wameitoa jana wakati walipotembelea Kituo cha Afya Ponge cha jijini Tanga
kwaajili ya Kufanya usafi kituoni hapo. Pia waligawa zawadi kwa wagonjwa
waliolazwa wodi ya watoto, wazazi na wanaume.
Kwa
upande wa mlezi wa chama hicho Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendego amesema
kuwa huo ni mfano mzuri na kwamba ataendelea kuwaongoza vyema wanahabari hao
kuijali na kuhudumia jamii ili waondokane na dhana kuwa wanahabari ni watu wa
kuogopwa.
erikali imepiga marufuku
ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa
kuomba kibali kwajili ya kukata mti huo.
Akizungumza wilayani
Siha juzi ,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba
Tanzania inawez a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa
bidhaa za miti unaofanyika nchini .
“Tukiendelea kukata miti
kma hivi tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba
niseme rasmi kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda
nyumbani kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu. Tunatakiwa
kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu” alisema
Nyalandu alisema kasi ya
ukataji miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kw aidadi ya
watu na kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa hakuna
jitihada za kurejesha iliyoondolewa.
“Kwa kaddri siku
zinavyozidi kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa
inavunwa kw azaidi ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa,
lazima tufanye jitihada zaidi kukomesha tatizo hili”.
Aliwaagiza wakuu wa
wilaya za Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa hadidu za rejea
kwa ajili ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya
kuanzisha mfuko huo.
Mtendaji Mkuu wa wakala
wa misditu (TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi
za wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi kuivamia
kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.
Alisema kwamba kwa msitu
wa asili kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya
kuoandwea huwa wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu ambacho
alishauri umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana na
ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.
Waziri Nyalandu alitoa
maagizo ya kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili
kufanywa wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya kuni
kama nishati na kulinda misitu.
“Umemem ni nishati
mbadala badala ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti
michache ikatwe ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo
waache kutumia kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati mbadala”
alisema.
WAZIRI MKUU Mizengo
Pinda atatuma wataalamu wa sekta ya kilimo ili waje kufuatilia suala la
mahitaji ya trekta ili kuziba pengo la mahitaji yake nchini Tanzania.
Alisema lengo la
Serikali la kuanzisha sera ya Kilimo Kwanza lilikuwa ni kuwasaidia wakulima
kupata ruzuku ya pembejeo, mbegu bora, na dawa za mifugo ili waweze kuongeza
ushalishaji.
“Kutokana na mkopo wa
Serikali ya India, tulipata matrekta 1,846 ambayo hayakuchukua muda kuisha.
Sasa hivi tunatafuta wabia wengine wa kutupatia zana za kisasa za kilimo kwa
sababu matunda yake mazuri tumeyaona, tunataka kilimo cha Mtanzania,” alisema.
Jana asubuhi (Ijumaa,
Oktoba 24, 2014), Waziri Mkuu alitembelea kampuni ya Farmers inayotengeneza
vipuri pamoja na matrekta ya kulimia na kuvuna yenye ukubwa wa Horse Power
80 na 72 ambayo alielezwa kwamba yanavumilia hali ya udongo mgumu wa Afrika.
Akitoa taarifa kwa
Waziri Mkuu, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Farmer, Bw. ZDZISLAW ZUKIEWICZ alisema
vifaa vinavyotengenezwa na kampuni hiyo vina waranti ya miaka saba na vinaweza
kuhimili udongo wa miamba na mawe wa ardhi ya Tanzania.
Kampuni hiyo
inatengeneza matrekta, mashine za kuvuna mazao shambani (combined harvester),
mashine za kukata nyasi za malisho ya mifugo pamoja na vipuri vyake. Alisema
bei ya trekta ni wastani wa Euro 22,000 na wako tayari kuleta vifaa hivyo
Tanzania kama watapewa oda.
Waziri Mkuu amemaliza
ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na
Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara
wa jiji la Warsaw.
No comments:
Post a Comment