Kifo chake
kimetokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi
hiyo.
Mwanasiasa
huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama
chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati
huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani
kwa miaka ishirini.
Michael
Chilufya Sata alizaliwa mwaka 1937 katika mji wa Mpika, eneo ambalo lilikuwa
wakati huo ni Northern Rhodesia. Muumini wa dini ya Kikristo ya madhehebu ya
Katoliki, alifanya kazi kama afisa polisi, mfanyakazi wa reli na mwanachama wa
chama cha wafanyakazi wakati wa utawala wa kikoloni. Baada ya Zambia kupata
uhuru wake, pia aliishi kipindi fulani mjini London, akiwa mfanyakazi wa reli,
na kurejea Zambia, akiwa na kampuni ya teksi.
Akiwa mwenye
sauti ya mkwaruzo yakiwa ni matokeo ya kuvuta sigara kwa muda mrefu, Bwana Sata
aliibuka katika siasa na kupata umaarufu katika miaka ya 1980.
Haraka akapata
sifa ya kuwa gavana mwenye kuchapa kazi kwa bidii, wakati akiongoza jimbo la
Lusaka na mtu wa utekelezaji kwa vitendo.
Lakini pia
alijulikana kama mtu wa kutoa amri, mtu asiyeendekeza urafiki na mkali- na
wapinzani wake walisema jina alilopewa la bandia la "King Cobra"
alikuwa anastahili kuitwa hivyo.
Kwa mara ya
kwanza alionekana kama mtu ambaye angetekeleza ahadi za kupambana na rushwa na
kupata ufumbuzi wa tatizo la ajira na kuleta ustawi wa jamii. Lakini kipindi
chake madarakani kiligubikwa na kuuzima upinzani wa kisiasa na kudorora kwa
uchumi.
Bwana Sata ni
rais wa pili wa Zambia kufariki dunia akiwa madarakani.
No comments:
Post a Comment