MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Sunday 26 October 2014

WANAHABARI WATAKIWA KUJIHUSISHA SHUGHULI ZA KIJAMII ILI KUIBUA CHANGAMOTO KWA NJIA RAFIKI

CHAMA cha waandishi wa Habari Wanawake TMWO Mkoa wa Tanga kimetoa rai kwa wanahabari wengine kote nchini kujihusisha moja kwa moja kwenye shughuliza kijamii ili kuweza kugundua changamoto zao kwa njia ya kirafiki.

Waandishi wengi wa Habari wamekuwa na mazoea ya kuandika habari kwenye matukio maalumu au kufanya uchunguzi baada ya kupokea ruzuku huku wakisahau kuwa kuna ushirikiano mzuri unaopatikna kwenye kutoa taarifa kama watajihusisha na wanajamii kuwa sehemu yao.

Rai hiyo wameitoa jana wakati walipotembelea Kituo cha Afya Ponge cha jijini Tanga kwaajili ya Kufanya usafi kituoni hapo. Pia waligawa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa wodi ya watoto, wazazi na wanaume.

Kwa upande wa mlezi wa chama hicho Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendego amesema kuwa huo ni mfano mzuri na kwamba ataendelea kuwaongoza vyema wanahabari hao kuijali na kuhudumia jamii ili waondokane na dhana kuwa wanahabari ni watu wa kuogopwa.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Pongwe Dkt Feisal Ally mwenye koti jeupe akitoa maelezo kwa Umoja wa Waandishi wa Habari Wanawake TMWO mbele ya mlezi wao Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendego mwenye jezi ya Kijani



Mwenyekiti wa TMWO Bertha Mwambela akifafanua jambo muda mfupi walipowasili kituo cha Afya Pongwe


Hapa Shughuli za Usafi zikiendelea kwenye kituo cha Afya Pongwe
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dendego, Uongozi wa Kituo cha Afya na wanachama wa TMWO katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment