WAZIRI MKUU
Mizengo Pinda atatuma wataalamu wa sekta ya kilimo kufuatilia suala la
mahitaji ya trekta ili kuziba pengo la mahitaji yake nchini Tanzania.
Alisema
lengo la Serikali la kuanzisha sera ya Kilimo Kwanza lilikuwa ni kuwasaidia
wakulima kupata ruzuku ya pembejeo, mbegu bora, na dawa za mifugo ili waweze
kuongeza ushalishaji.
“Kutokana
na mkopo wa Serikali ya India, tulipata matrekta 1,846 ambayo hayakuchukua muda
kuisha. Sasa hivi tunatafuta wabia wengine wa kutupatia zana za kisasa za
kilimo kwa sababu matunda yake mazuri tumeyaona, tunataka kilimo cha
Mtanzania,” alisema.
Jana
asubuhi (Ijumaa, Oktoba 24, 2014), Waziri Mkuu alitembelea kampuni ya Farmers
inayotengeneza vipuri pamoja na matrekta ya kulimia na kuvuna yenye ukubwa wa Horse Power 80 na 72 ambayo
alielezwa kwamba yanavumilia hali ya udongo mgumu wa Afrika.
Akitoa
taarifa kwa Waziri Mkuu, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Farmer, Bw. ZDZISLAW
ZUKIEWICZ alisema vifaa vinavyotengenezwa na kampuni hiyo vina waranti ya miaka
saba na vinaweza kuhimili udongo wa miamba na mawe wa ardhi ya Tanzania.
Kampuni
hiyo inatengeneza matrekta, mashine za kuvuna mazao shambani (combined
harvester), mashine za kukata nyasi za malisho ya mifugo pamoja na vipuri
vyake. Alisema bei ya trekta ni wastani wa Euro 22,000 na wako tayari kuleta
vifaa hivyo Tanzania kama watapewa oda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland jijini Warsaw akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Waziri Mkuu
amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi
alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya
wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.
No comments:
Post a Comment