MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Tuesday 21 October 2014

JE, WAJUA? KATIKA SEHEMU FULANI, KARIBU ASILIMIA 85 YA NAFASI ZA KAZI HAZITANGAZWI


JE, WAJUA . . .?
● Je umewahi kujiuliza kwa nini unahitaji kuchuma pesa?
● Ni magumu gani utakayokabili ukipata kazi?
● Ni nini kinachoweza kukusaidia kuwa na maoni yenye usawaziko kuhusu pesa?

Baadhi ya mitazamo ya upande mmoja inaona kuwa, kufanya hima na kujitahidi ni mambo ambayo yanaishia tu katika kukidhi mahitaji ya kidunia na maisha ya kimaada ya mwanaadamu na baadhi ya maktaba zingine za kifikra zina mitazamo tofauti. 

Ukweli wa mambo ni kuwa, kazi na kufanya hima katika jamii yoyote ile na katika mtazamo wa dini na maktaba na pote lolote lile la kifikra ina maana na nafasi maalumu.

Ni kweli kwamba katika sehemu fulani za ulimwengu, vijana wanalazimika kufanya kazi kwa saa nyingi ili kusaidia familia zao. Hata hivyo, ikiwa hali yako ni tofauti, mbona upoteze usawaziko wako? Kulingana na wataalamu wengi, kufanya kazi kwa zaidi ya saa 20 kwa juma huku ukiendelea na masomo kunaweza kusababisha madhara. Wataalamu wengine wanapendekeza wanafunzi wasifanye kazi kwa zaidi ya saa nane hadi kumi kwa juma. Mfalme Sulemani mwenye hekima alisema: “Konzi moja ya pumziko ni afadhali kuliko konzi mbili za kazi ngumu na kufuatilia upepo.”—Mhubiri 4:6.

Yesu alisema kwamba wenye furaha ya kweli ni wale “wanaotambua uhitaji wao wa kiroho.” (Mathayo 5:3) Pia alisema: “Hata wakati mtu ana vitu vingi uzima wake hautokani na vitu alivyo navyo.” (Luka 12:15) Kijana Mkristo anayeitwa Maureen, anatii shauri hilo. Anasema: “Sitaki kunaswa na miradi ya kufuatia vitu vya kimwili. Ninajua hali yangu ya kiroho itaathirika nikinaswa na mtego wa kutafuta pesa tu.”

Kumbuka, “nguvu za udanganyifu za utajiri,” zinaweza kusonga upendezi wako wa mambo ya kiroho. (Marko 4:19) Kwa hiyo, ukiamua kufanya kazi baada ya shule ili upate pesa, panga ratiba yako ili utangulize mambo ya kiroho. Mwombe Yehova akusaidie. Anaweza kukupa nguvu za kukabili hali hiyo na kukusaidia kuendelea kuwa na usawaziko wa kiroho.

Je Utaendelea kukaa nyumbani ukitamani kupata kazi? Hapana, Ndio! Hata mtu mvivu atake kitu namna gani, hatakipata kamwe. Mwenye bidii atapata kila kitu anachotaka.Methali 13:4

Will Durant mwandishi wa Kimagharibi wa kitabu cha Historia ya Ustaarabu anasema kuwa: "Afya na uzima vipo katika kufanya kazi. Kufanya kazi ni moja ya mambo ya nembo za furaha ya mwanaadamu katika maisha. Kwa mtazamo wangu, ni bora tumuombe Mwenyezi Mungu tawfiki ya kufanya kazi badala ya kuomba mali na utajiri."

Kuwa na hima na kufanya kazi udharura na umuhimu wake ni kama vile maji na chakula katika maisha ya mwanaadamu. Kimsingi, dhati ya mwanaadamu huelekea katika hima na kufanya kazi. 

Hata hivyo swali la kimsingi la kujiuliza ni kuwa, mwanaadamu anafanya kazi kwa ajili ya lengo gani? Je mwanaadamu anafanya kazi kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya kimaada na kwa ajili ya kuboresha maisha yake? Je mwanaadamu anakula na kunywa ili apate nguvu ya kufanya kazi? Au anafanya kazi ili aweze kula vizuri na kuwa na maisha mazuri na bora? Maswali haya na mengineyo tutayajibu katika kipindi chetu kijacho.

Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu kwa maji na udongo, kisha akampulizia roho na kumtaka afanye hima na bidii pamoja na amali njema ili aweze kuwa khalifa na kiongozi Wake katika ardhi. 

Mwenyezi Mungu anasema katika aya ya (29 ya Surat ar-Rahman:)
"Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo."

Hivyo basi kukaa bure, kutofanya kazi na kutokuwa na malengo ni mambo ambayo hayana nafasi katika ulimwengu huu na Uislamu unayapiga vita haya. Kila kilichomo katika ulimwengu huu, yaani viumbe wote, miti na mimea vinafanya kazi zao kwa mipango na utaratibu maalumu. 

Viumbe vyote vinafanya harakati kwa nidhamu na mpango maalumu na makini kuelekea katika lengo maalumu. Kwa muktadha huo, mwanaadamu naye akiwa kiumbe bora kabisa wa Mwenyezi Mungu katika mgongo wa ardhi anapaswa kwenda sambamba na nidhamu na mipango hii.

No comments:

Post a Comment