MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Sunday, 28 December 2014

MAHAKAMA YADAIWA KUITESA FAMILIA YA WATU 18 MOROGORO



  FAMILIA ya watu 18 wakiwemo watoto 10 na akina mama Nane mtaa wa Juma 50 kata ya Mwembesongo eneo la Mafisa Msamvu Kilabu cha Makondeko Manspaa ya Morogoro wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko na uambukizo baada ya kutupiwa vitu vyao nje ya nyumba kwa madai ya amri ya mahakama.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani  hapo, baadhi ya wanafamila hao Magreth Kainyingi  na Adistela Kainyingi walisema tukio hilo walichofanyiwa Desemba 23 limelenga kuwadhalilisha,kuwafedhehesha na kuwadhoofisha kimaendeleo kwakua hapo ni kwao kihalali.

Walisema chimbuko la mgogoro huo ni deni wasilolitambua la shilingi 800,000 walilokopeshana kati ya baba yao na mtu waliemtaja Josia Masini aliebadili dhana ya mkopo nakuwa malipo ya ununuzi wa nyumba hiyo.

Katika ufafanuzi huo Magreth alisema mbali na vielelezo vya hati miliki walivyonavyo katika eneo hilo Ploti namba 35 kitalu ‘A’Msamvu,na kuthibitishwa na vyombo vya usimamizi ikiwemo Manspaa bado Mahakama imekuwa ikipinga uhalali wake na kumpatia haki Masini.

Wakizungumzia kutupwa nje kwa mizigo yao walisema Desemba 23 walivamiwa na watu wasiowajua waliojitambulisha kuwa wafilisi wa mahakama kisha kuanza kubeba mizigo na kuitoa nje huku wakiwataka kulipa shilingi 900,000 kama usumbufu.

Kwa nyakati tofauti imefikia Masini akishirikiana na uongozi wa mtaa amekuwa akiwakamata kuwafikisha polisi na mahakamani na tayari alishawahi kuwafunga jela mwaka mmoja na kazi ngumu wakiwa na watoto wadogo.

MISS TANZANIA YAFUNGIWA KWA MIAKA MIWILI


SERIKALI ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.
 
Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.

Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.

Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.

Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.

Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika

Saturday, 27 December 2014

WAWILI WAUAWA TANGA MSIMU WA SIKU KUU



·       JESHI la Polisi Mkoani  Tanga linatoa shukrani kwa wananchi kwa kutoa ushirikiano  mzuri  wa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu kipindi hiki cha Krismas  na hivyo  kuwezesha wananchi kusherehekea  kwa amani na utulivu . 

Akitoa taarifa ya hali ya uhalifu kwa waandishi wa habari akiwa ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Frasser Kashai amesema wanawaomba wananchi kuendeleza ushikiano huo ili kuweza kuvuka salama mwaka 2014 kwa amani.

Aidha Kamanda Kashai amesema kutokana hali ya uvunjivu wa amani kuendelea kuijtokeza katika maeneo mbalimbali mkoani hapa kumekuwa matukio yaliyojitokeza baadhi ya Wilaya za mikoa .

Amesema  watu wawili wamefariki katika matukio mawili taofauti ,ambapo amesema mnamo tarehe 26 majira ya saa moja kamili asubuhi huko maeneo ya Ndekai Kata ya Baga   Tarafa ya Mgwashi Kando ya barabara ya Baga –Kwemakame Wilaya Lushoto ,Mtu aliyefahamika kwa jina la Rshidi Kilua  mwenye umri wa miaka mkazi wa Ndekai ,aligundua mwili wa Mpwa wake aitwe Hashimu  Rajabu  ukiwa na majereha kichwani .

Hata kamanda amesema mwili marehemu umefanyiwa uchunguzi na madaktari na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Amesema chanzo cha mauaji hayo kinasakiwa kuwa ni Migogoro ya ardhi  ,ambapo mpaka sasa watu wawili ambao ni Waziri Salimu umri wa miaka 35 mkazi wa Ndekai Baga  wapili ni Ramadhani Ayub umri wa miaka 40 mkazi wa Mwangoi  Baga wamekamatwa kufauati mauaji hayo kwa ajili ya mahojiano .

Katika tukio njingine kama hilo Mtun mmoja aliye fahamika kwa jina la Husein Muamed amefariki Dunia wakati alipokuawa anapata matibabu katika Hospitali ya Bombo mara baada ya kokolewa wakati alipokuwa akishambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za uwizi baada ya kuvunja nyumba na kuingia ndani kwa nia ya kuiba .Kamanda Kashai amesema upelelezi unaendelea kufuatia tukio hilo ili kuwabaini  waliojichukulia sheria mkonani.

Katika hatua nyingine jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia  watu wapatao sita ambao ni ni Raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia Nchini bila kibali .

Kamanda Kashai amewataja watuhumiwa hao kuwani Gesamu Abato mwenye umri wa miaka 30,Hash Negash Grinanu umri wa miaka 20,Tsegaye Aliso umri wa miaka  21 ,Jamal Godso umri wa miaka 25 ,Alemayo Ataro umri wa miaka 22 na Erigudo Elitiro umri wa miaka 25 .

Kamanda Kashai amesema Watuhumiwa hao watafishwa mahakamani baada ya upelelezi wa awali kukamilika .

KIVUKO MTO KILOMBERO CHAKUSANYA MIL. 776



KATIKA kipindi cha miezi 11 mwaka huu kivuko cha mto Kilombero kimeadaiwa kukusanya shilingi MIL 776,229,336 katika makusanyo yake wakati wa uvushaji watu na magari.

Hayo yalisemwa na mkuu wa kivuko cha mto Kilombero Mhandisi Fadhil HarounMeneja kwa niaba ya Meneja wa Temesa mkoa wa Morogoro Mhandisi Magreth Mapula kwenye kikao cha bodi ya kivuko hicho kinachotoa huduma ya kuvusha watu na vyombo vya usafiri viendavyo na kurudi wilayani Ulanga.

Katika ufafanuzi wake Haroun alisema mapato yamekuwa yakiongezeka na kushuka kutokana na msimu huku akifafanua kuwa mwezi Machi na Mei mapato yamekuwa yakishuka kutokana na hali ya mvua kusababisha barabara kutopitika kwa urahisi watu wengi kuwa mashambani kwa kilimo.

kwa mujibu wa meneja huyo kunachangamoto ya mafuriko na uharibifu mkubwa wa miundombinu,magari kugonga kivuko na kutumbukia majini,majani na nyavu kujisokota kwenye mfumo wa usukani wa kivuko na mchanga kujaa mtoni kunakosababisha kina kupungua.

Kwa upande wao wajumbe wa bodi ya kivuko hicho akiwemo mbunge wa jimbo la Ulanga magharibi Dk Haji Mponda walimtaka wakala wa ufundi na umeme Temesa mkoa wa Morogoro kuharakisha ujenzi wa vibanda vya kujikinga na mvua na jua kivukoni hapo.

Aidha walikitaka kivuuko hicho kuongeza pato lake ili kiweze kumudu kugharimia changamoto zinazojitokeza na kukifanya kuwa na tija katika utendaji wake.

Wazo hilo liliungwa mkono na mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala akionyesha masikitiko yake ya jinsi ambavyo mawazo ya bodi hayatekelezeki na kukatisha tamaa bodi hiyo kwa ushauri wake.

Aidha waliutaka uongozi wa usimamizi kivukoni hapo kutoa nafasi kwa vyombo vya usafiri vyenye abilia kupewa kipaumbele kupita kwanza kabla ya maroli ya mizigo hasa inapotokea kunakuwa na foleni.

PROF. TIBAIJUKA APATA 'WENZA' SAFARI YA MAISHA MAPYA



KATIKA hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.

Waliotupwa nje kutokana na tuhumua za ufisadi ni pamoja na Anna Tibaijuka- aliyekuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi, Sospeter Muhongo-aliyekuwa waziri wa nishati na madini huku Lazaro Nyalandu akihamishwa kutoka wizara ya mali asili na italii aliyokuwa akihudumu.

Walioondolewa kwenye wizara zao za awali na kuhamishwa ni pamoja na Lazaro Nyalandu ambaye anarudi mazingira. Saada Mkuya Salum kutoka fedha na kuhamishiwa ikulu pamoja na Gaudensia Kabaka.Hayo ni baadhi ya majina niliyopata.

Aidha rais Kikwete amewaondoa baadhi ya mawaziri katika baraza lake kutokana na uwajibikaji hafifu ambao ni Chiza Christophera-kilimo, Maghembe Jumanne-maji, Hawa Ghasia-tamisemi na Mathias Chikawe-utumishi Kikwete pia amewaingiza wengine wapya kwenye baraza la mawaziri ambao ni Serukamba Peter, Deo Filikunjombe na Kigwangala Khamisi.Hao bado haijafahamika ni wizara zipi walizoteuliwa.

Pia wapo waliopanda cheo kuwa mawaziri kamili ambao ni Simbachawene George, Mwanri, Godfrey Zambi, Mwigulu Nchemba, January Makamba na Greyson Lwenge. Hawa taarifa kamili ya wizara watakazohudumia tutawaletea.
Inasemekana kuwa Kikwete amepangua na kulipanga upya baraza lake kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyotarajiwa. Pia atamteua mkuu mpya wa sheria wa serikali ndani ya siku tatu zijazo kama nilivyodokezwa.