WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia na sekta binafsi
katika mradi mkubwa wa usafirishaji abiria.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana wakati akifungua
Mkutano wa siku mbili wa Majadiliano
yenye lengo la kuutangaza mradi wa mabasi yaendayo kasi kwenye ukumbi wa
Mlimani City Pinfa amesema kutèkelezwa kwa mradi huo kutatoa fursa za ubunifu
utakaowezesha kupatikana suluhisho la usafiri mijini hasa inayokua kwa kasi
barani Afrika.
Amesema
ni matumaini ya Serikali kwamba wadau kutoka sekta binafsi ambao ni wazawa na
wa kutoka nje ya nchi watashiriki kwenye mradi huu ili uweze kuboresha matumizi
ya kadi ambayo mtu hatatakiwa kulipia fedha taslimu akiwa ndani ya basi bali
kutumia kadi anayoilipia kabla ya kuingia ndani ya basi husika.
Mapema,
akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(TAMISEMI), Hawa Ghasia amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo
unafanikiwa na kushukuru Benki ya Dunia
ambayo imetoa dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kufadhili mradi huo.
Mkutano
huo unawashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa ndani na wa nje wanaotarajiwa
kutoa huduma za mabasi makubwa na madogo, utoaji tiketi, ulinzi, usafi na
huduma za maduka.
No comments:
Post a Comment