JESHI la polisi mkoani Tanga linamshikilia kijana Said Abdalah mwenye
umri wa miaka 32 mkazi wa Kwanjeka mjini hapa kwatuhuma za kukamatwa na madawa yanayoyo dhaniwa
kuwa ya kulevya aina ya heroin yenye
uzito wa kilogram moja.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Costantine Masawe |
Mtuhumiwa huyo amekamatwa mnamo juni 4 majira ya saa nane mchana.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani
Tanga, ACP Costantine Masawe akiwa ofisini kwake amesma mtuhumiwa ambaye pia ni mfanya biashara wa Makorora mjini
humu amekamatwa kupitia taarifa zilizotoka kwa raia wema.
Kamanda Masawe amesema baada ya taarifa ndipo askari walifika eneo
alipokuwamtuhumiwa na kumkamata na kwamba mpaka sasa thamani ya madawa hayo
haijatambulika hadia mkemia wa serikali
atakapotoa uthibitisho wa dawa hizo na uzito wake halisi.
Masawe amesema wakiwa katika harakati za kushughulikia suala hilo watu
wawili Amri Mohoreja mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Donge na Hassan Mwandani mwenye
miaka 24 mkazi wa Mikanjuni walitaka kuwashawishi maofisa Polisi kupokea rushwa
ya shilingi 8,600,000 ili wapindishe ukweli na kumwachia mtuhumiwa.
Amesema watu hao baada ya kusikia kukamatwa kwa mwezao Said Abdala
mtuhumiwa wa madawa hayo ya kulevya waliwasiliana kwa njia ya simu na maafisa
wa polisi ambao waliwekeana miadi ya kukutana eneo la Harbours Club.
Mtu aliyeathiriwa na utumiaji wa dawa vya Kulevya |
Taratibu za kisheria zinaendelea ili watuhumiwa kufikishwa
mahakamani huku akiwapongeza askari wake kwa kukataa kupokea rushwa na kuitaka
jamii kuzidi kushirikiana nao kufichua wanaousika na uhuzaji na utumiaji wa
madawa ya kulevya nchini.
No comments:
Post a Comment