MKOA wa Dodoma umetajwa kuongoza
kitaifa kwa kuwa na tatizola watoto wa mitaani kwa kiwango
cha asilimia 13.3.
Takwimu hizo zimeainishwa
mjini Dodoma na katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Dodoma ndugu Deogratius Yinza katika kikao cha wadau cha kujadili tatizo la watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi na watoto wa mitaani.
Amesema mkoa wa Dodoma una ongezeko
kubwa la watoto hao ambapo wilaya zinazoongoza kwa mkoa wa Dodoma ni
wilaya ya Bahi ikifuatiwa na wilaya ya Chamwino na Mpwapwa.
Amesema takwimu za kimkoa za mwaka
jana kuanzia januari hadi disemba zinaonyesha kuwa Dodoma ina watoto wa
mitaani 49,829 ambapo kati ya hao wavulana nio 25,860 na wasichana ni 23,968.
Ametaja sababu kubwa ya ongezeko
hiloni sababu ya kibinadamu ambapo familia nyingi zimekosa muelekeo na
kusababisha kutelekeza familia zao,kutumikishwa na ukatili wa kijinsia.
Yinza ametoa wito kwa wadau kutambua
changamoto zilizopo katika tatizo hilo ili waweze kupambana kupunguza tatizo
hilo na kusisitiza wadau kuzitambua sheria zinazomlinda mtoto na kuzitekeleza
kulingana na mikataba ya kisheria iliyopo.
Ametaka kukomeshwa kwa mila
zilizopitwa na wakati ambazo zinawakandamiza watoto na kuwabagua kulingana na
jinsia zao na kuwafuatilia wazazi na walezi kama wanatoa haki na stahili kwa
watoto wao ili watakaokaidi wachukuliwe hatua.
No comments:
Post a Comment