WATU wanaodhaniwa kuwa majambazi wapatao
nane wakiwa na silaha mbalimbali za jadi wamemvamia na kumopora fedha mfanyabiashara
mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Mfanyabiashara
huyo ambae ni mkazi katika kijiji cha Jasini wilayani Mkinga alitambuliwa kwa jina la Mohamed
Tembo 30. Watu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga kuhusiana na
Tukio hilo.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Costantine Masawe amethibitisha tukio hilo na kusema
kuwa Tembo alivamiwa usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7:30 usiku ambapo pia walifanikiwa
kutokomea na fedha taslimu sh 978,600/=.
Katika tukio
jingine la June 8 mwaka huu majira ya Saa 2:30 usiku huko Pingoni Mjohoroni Pande
Mkoani hapa, Sixmudi Kakurumu 62 mkazi wa Pande amevamiwa na watu wasiojulikana
na kumjeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumpora sh 400,000/=.
Watu hao
wapatao nane waliokuwana na silaha za jadi ikiwemo mapanga na marungu walipora
pia vitu mbalimbali vya dukani ambavyo thamani yake haikuweza kufahamika mara
moja
Kamanda
Masawe amesema wanaendelea kufanya juhudi za kuwapata watuhumiwa hao wakati
Kakurumu akiendelea kuuguza majeraha katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo.
No comments:
Post a Comment