MAMLAKA ya Mapato Nchini TRA
imeshindwa kufikia lengo la makusanyo ya mapato kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo mapato pungufu ya kodi kuliko ilivyotarajiwa ikiwemo makampuni ya
madini.
Akiwasilisha leo makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2014/2015, Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum amesema hadi kufikia April mwaka huu mapato halisi ya kodi yamefikia sh. bilioni 7,771.5.
Amesema kiasi hicho ni sawa na asilimia 75 ya lengo la mwaka la kukusanya sh. bilioni 10,395.4 kiasi mbacho kilichangiwa zaidi na kodi ya ongezeko la thamani , kodi ya kampuni na kodi ya mapato ya ajira ambazo kwa pamoja zimechangia kiasi cha asilimia 80.
Saada amesema kutofikia kwa lengo la makusanyo hayo pia kumechangiwa na kushuka kwa makusanyo hususani kodi ya zuio kutokana na kupungua kwa makusanyo katika shughuli za utafiti wa gesi na mafuta.
Amesema sababu nyingine ni pamoja na
kufutwa kwa Tozo ya kadi ya simu na makusanyo hafifu kutoka kwenye Ushuru wa
bidhaa.
Waziri huyo amesema kwa upande wa
forodha, sababu zilizochangia kutofikiwa kwa lengo la makusanyo ni ukuaji
mdogo wa uingizaji wa bidhaa kutoka nje na ongezeko la kuingiza bidhaa kupitia
njia zisizo rasmi na bandari bubu.
Akizungumzia udhibiti wa Fedha
haramu na Ufadhili na Ugaidi, Waziri Mkuya amesema Wizara inaendelea kuratibu
zoezi la kutahimini mianya na viasharia vya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi
katika sekta mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment