MSAFARA wa mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Singida umeingia
dosari ukiwa katika siku yake ya kwanza baada ya kutokea ajali inayohusisha
magari matatu, yakiwemo mawili ya polisi, kwenye kijiji cha Kirumbi, mpakani
mwa mkoa wa Tabora na Singida.
Kwa mujibu wa mashuhuda kutoka eneo
la ajali, ajali hiyo imetokea muda wa saa 6.30 mchana ambapo inadaiwa gari STK
3288 lililokuwa limewabeba wahudumu wa afya kuliparamia kwa nyuma gari la
polisi namba PT 1980.
Gari hilo lenye usajili PT 1980
lililazimika kusimama ghafla kutokana na gari lingine la polisi namba PT
2010 lililokuwa mbele yake kupata pancha na kusimama katikati ya barabara.
Mashuhuda hao wamedai kuwa mara
baada ya kutokea kwa ajali hiyo, askari polisi watatu waliokuwemo kwenye gari
namba PT 1980 waliumia sehemu mbalimbali za miili yao, ikiwemo kuvunjika
mikono na miguu, na mmoja wao hali yake ni mahututi.
Askari wote watatu wamepelekwa
hospitali ya Rufaa ya St, Gasper Itigi kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment