JESHI
la polisi mkoani humu linamshikilia
Daktari wakituo cha afya cha tumaini Richard Kafuru mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa Majengo kwa tuhuma za kukutwa na
nyaraka hewa za bima ya afya ofisini kwake.
Akitoa ufafanuzi juu ya
tuhuma hizo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Juma Ndaki
amesema Daktari huyo amekamatwa
kupitia taarifa zilizotolewa na muuguzi na msimamizi wa kituo hicho Sir.Flora
Mushi mwenye umri wa miaka 48 mkazi wa
chumba geni jijini humu.
Amesema muuguzi huyo aligundua majina
mbalimbali ya hewa ya wagonjwa waliotibiwa mwezi wa januari mwaka huu visivyo
halali kwa kutumia bima ya afya.
Aidha kaimu kamanda huyo amesema
nyaraka hizo ni Kadi 15 zenye namba na majina tofauti, Hati za kuchukulia dawa
kituoni hapo na maduka ya dawa yaliyoidhinishwa na bima ya afya, ambapo
alitumia majina ya madaktari wenzake katika fomu hizo.
Hata hivyo amesema mtuhumiwa huyo
alikutwa na madaftari sita ya wagonjwa ambayo ni kinyume na taratibu ya bima ya
afya wanapoingia mkataba wa vituo vya afya au maduka ya kutolea madawa.
Sanjari na hayo Ndaki amesema
uchunguzi wa awali umebaini hasara
ya shilingi milioni 45 katika kituo hicho ambapo
mtuhumiwa huyo ambaye ni daktari anashikiliwa na jeshi la polisi kwa hatua
zaidi.
Akizungumza kwaniaba ya msimamizi wa
kituo hicho Sir Alfonsina Sangawe
amesema ni kwel daktari huyo
amefanya kosa la kudhalilisha kituo pamoja na kanisa, hivyo wamemfukuza kazi na
hatakuwa mtumishi tena kituoni hapo.
No comments:
Post a Comment