KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja anaesadikiwa kuwa mkaazi wa mji wa
Pongwe jijini Tanga ambaye hakuweza kutambulika mara moja amejifungua mtoto mwenye
jinsia ya kike kisha muda mfupi baadae kumtupa chooni.
Tukio hilo la kinyama na la
kusikitisha limetokea usiku wa Juni 12 ambapo watu wengi walikuwa makini kwenye
luninga zao kufuatilia mchezo wa kwanza wa michuano ya kombe la Dunia unaoendelea
nchini Brazil.
Muonekano wa Choo hicho kwa nje
Wakizungumza mwanamkemakini.blogspot.com
wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa wamefanya jitihada za kumnusuru mtoto huyo
licha ya kuwa hadi sasa mtuhumiwa hajatambulikana.
|
| |
Nae Balozi wa mtaa wa Misufini Mohamed
Mbogo amekiri kupokea taarifa hizo alizozipata asubuhi ya majira ya saa 1:30 Juni
13 kutoka kwa Polisi Jamii.
|
No comments:
Post a Comment