UMOJA wa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda
na waendeshaji wa bajaji mjini hapa (UWAKIBATA) wametakiwa kuendelea kuitii
sheria za usalama barabrani ili kuepukana na ajali zinazotoke mara kwa mara.
Hayo ameyasema Kamanda wa kikosi cha
usalama barabarani Mkoani Tanga, Abdi Isango kwenye mkutano wa uchaguzi wa
viongozi mbalimbali wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Polisi, (police
mess) mjini hapa.
Aidha Isango ameeleza kuwa chaguzi
huo ni ili madereva hao wapate kutambua umoja wao ambao viongozi wake watakuwa
na jukumu la kusaidiana na Jeshi hilo kuangalia usalama wa madereva hao.
Hata hivyo amesema chama kwa
kushirikiana na jeshi la polisi watahakikisha kuwa waendesha bodaboda wanazitii
sheria zilizowekwa na viongozi wao na wale ambao watahusika na uvunjaji wa
sheria hizo watachukuliwa hatua.
Kwa upande wake mwenyekiti ambaye
amechaguliwa kwenye uchaguzi huo Daudi Bilali amesema anatarajia juona madereva
hao wanaendelea kuitii sheria ili kuisaidi serikali majukumu.
Sambamba na hayo amewomba waendesha
bodaboda kutoa elimu kwa abiria juu ya uvaaji wa kofia ngumu za element ili
kuondoa wasiwasi wa kupatwa na maradhi.
No comments:
Post a Comment