MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Saturday 14 June 2014

WAKALA WA MIRUNGI AMPONZA KIJANA




JESHI la polisi mkoani hapa lina mshikilia kijana Kassimu  Athumani mkazi wa barabara ya 21 jijini Tanga kwa kukamatwa na mirungi yenye kilogram 100  na bunda 119 akisafirisha kutoka Tanga kwa kutumia fuso yenye  namba za usajili  T213 BSG kwenda  Dar es salaam.

Akiongea na mwanamkemakini.blogspor.com kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa3 asubuhi  eneo la Mkata wilaya ya Handeni.

Kanda Masawe amesema kijana huyo alikiri kupatiwa mirungi hiyo na mtu mmoja Tanga ili awapitishie wahisika eneo la Chalinze, Kibaha na jijini  Dar es salaam.

Aidha kamanda massawe amesema licha ya kuwa nchi za jirani zimeruhusu matumizi ya bangi lakini bado nchini jeshi hilo litaendelea kupambana na wanaojihusisha na uuzaji pamoja na matumizi hayo. Taratibu za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zinaendelea.

Katika tukio jingine mtoto mmoja ambaye ameitambulika kwa jina la Junior Salvatory (4) mkazi wa Kikunde amefariki dunia mara baada ya kugongwa na pikipiki.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda massawe amesema Salvatory amegongwa na mwendesha pikipiki namba za usajili T649BGS aina ya Sun L G Mathias  Yohana mwenye umri wa miaka 49.

Aidha amesema mototo huyo aligongwa huko kijiji cha Tonguni mnamo juni 11 majira ya saa11 za jioni.

Sambamba na hayo ametoa wito kwa wale wote watakao kamatwa na madawa ya kulevya kuwa jeshi la polisi litapambambana nao hadi hatua ya mwisho na amewataka walezi wawatoto wasiwaachie watoto wakizurura barabarani hali ambayo inaweza ikahatarisha maisha yao.

No comments:

Post a Comment