MFANYABISHARA mmoja mkazi
wa Michungwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Ally Rajabu Makufya 72, amejiua
kwa kujipiga risasi ya shingo kwa kutumia bunduki.
Marehemu
ambaye pia ni mmiliki wa baa mbili wilayani Muheza amejiua June 8 majira ya saa
3; 30 asubuhi akiwa chumbani kwake akitumia bunduki yake anayoimiliki kihalali.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga amethibitisha tukio hilo.
Wakati huohuo
June nane majira ya saa 8:20 mchana watu wa wawili Jofrey Daniel (20) mkazi wa
kwanjeka na Musa Hamisi miaka 44 mkazi wa Mtambwe Mkoani hapa wamekamatwa
wakiwa na bunduki Raifo yenye namba 2703520 iliyowahi kuripotiwa na Musa Hamisi
44 kwamba imeibiwa.
Watu
hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamekamatwa maeneo ya Ngomeni barabra kuu
ya Muheza -Tanga pia wakiwa na risasi mbili za bunduki hiyo, ganda moja la
risasi, panga moja, kisukimoja na bisi bisi mbili.
No comments:
Post a Comment