Tanzania
imeshika nafasi ya pili kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande wa
mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya jana (Mei 29
mwaka huu) kuilaza Afrika Kusini mabao 2-0.
Mechi
hiyo ilichezwa Uwanja wa SSKB jijini Gaborone ambapo kwa matokeo hayo Tanzania
imetwaa medali ya fedha baada ya kushika nafasi ya pili. Nigeria ndiyo ilishika
nafasi ya kwanza na kutwaa medali ya dhahabu.
Tanzania
imemaliza ikiwa na pointi kumi ambapo ilishinda mechi tatu, sare moja na
kupoteza moja mbele ya Nigeria.
Katika
mechi ya kwanza ilitoka sare ya bao 1-1, ikawafunga Botswana 2-0, Swaziland
wakachapwa 3-0 na baadaye kuwafunga Afrika Kusini 2-0. Timu ya Tanzania
inayofundishwa na kocha Abel Mtweve ilifungwa na Nigeria mabao 2-0.
Wachezaji
16 waliounda kikosi hicho cha Tanzania katika michezo hiyo inayomalizika leo (Mei
30 mwaka huu) ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani,
Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo,
Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na
Thomas Chindeka.
Nchi
nyingine zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika
Kusini, Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland wakati Gabon na Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) zilijitoa dakika za mwisho.
No comments:
Post a Comment