Ester Bulaya, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Mara na Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira |
KAMATI ya Kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imesema hairidhishwi na mkakati wa
utekelezaji wa Mradi wa Kigamboni.
Kamati hiyo imefikia
hatua hiyo toka mchakato huo uanze kumekuwa na changamoto nyingi ikiwa ni
pamoja na malalamaiko ya wakazi wa eneo husika .
Kauli hiyo imetolewa
leo na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Ester Bulaya alipokuwa akisoma
taarifa ya kamati hiyo kwa kusema kumekuwa na malalmiko mengi toka kwa wananchi
wa eneo hilo kuwa mchakato huo wa uandaaji wa mpango kabambe wa mji mpya
haukuzingatia sheria ya mipango miji namba 8 ya mwaka 2007.
Ester Amesema mbali
ya kutofuatwa kwa sheria hiyo pia wananchi wa eneo hilo walikatazwa kukarabati
na kufanya shughuli za kimaendeleo katika maeneo yao huku utekelezaji wa
mchakato huo kuwa wa muda mrefu kiasi cha kukatisha tama.
Amesema kutokana na
changamoto hizo kamati yake inaitaka Serikali kuanza mara moja kukamilisha
maandalizi ya mpango kabambe na kuanza utekelezaji wa mradi.
No comments:
Post a Comment