·
Ramani ya Mkoa wa Tanga
WAFANYA biashara wa mazoa ya nafaka na
samaki waliopo barabara ya 15 Kata ya Ngamiani Kusini mijni hapa, wameiomba Halmashauri
ya jiji la Tanga kusimamia usafi wa mifereji iliyopo kandokando ya barabara
hiyo ambayo imekuwa chanzo kikuu cha
kuwepo kwa magonjwa ya milipuko pamoja mazalia ya mbu hususani kipindi cha mvua.
Wakizungumza na Redio huruma ya Mkoani Tanga kwa
nyakati tofauti Akida Ramadhani na Kimaro Gilioni wamesema
wao wamekerwa na hali ya uchafu uliopo ndani ya mifereji hiyo ambayo inasababisha maji machafu kutuama
jambo amablo linahatirisha afya wakazi
wa eneo hilo.
Wafanya biashara hao wameiomba Halmashuri
kuchua hatua ya kusafisha mifereji hiyo
ili maji yapite kwa uraisi badala ya wafanya biashara kuhangaika wenyewe
kuwatafuta vibarua na kuwalipa wenyewe kwa muda mrefu.
Akilizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa Mtaa wa Jamhuri Kata ya Ngamiani Kusini, Shaban
Choyo amesema kuwa ni wajibu wa kila
mfanya buiashara kusimamia usafi katika eneo hilo hali ambayo itasaidia kuondokana na magonjwa ya mlipo kama Dengue
na mengineyo.
Amesema yeye kwa kushirikiana na
viongozi wengine wa kata watahamasisha jamii zaidi juu ya usafi huo wa mifereji kama wanavyo fanya katika maeneo mengine ikiwemo
barabarani.
· KATIKA TUKIO JINGINE
WANANCHI wametakiwa kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabrani ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara mkoani hapa.
WANANCHI wametakiwa kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabrani ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara mkoani hapa.
Akizungumza na radio huruma cha Mkoani Tanga leo katika kipindi cha tungumze
asubuhi askari wa kikosi cha usalama wa barabarani PC IMANI mesema nivyema kila
mwananchi atambue umuhimu wa kujua alama za vivuko wanapo kuwa barabarani.
Amesema vivuko hivyo vya barabarani ambavyo ni punda milia, vivuko vinavyoongozwa
na taa za barabarani na vivuko vinavyoongozwa na askari wa polisi
endapo vitafuatwa kwa usahihi kwa asilimia kubwa vinaweza kuondoa ajali za
barabarani.
Sanjari na hayo ametoa rai kwa wananchi kushirikiana
na jeshi la polisi katika kuwapa taarifa zinazo husu uvunjifu wa sheria za barabarani.
No comments:
Post a Comment