MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Friday, 30 May 2014

KATIBU UDP MOROGORO AFARIKI DUNIA

KATIBU wa chama cha United Democratic Party UDP mkoa wa Morogoro Ununi Mn’goo (61) amefariki dunia May 28 nyumbani kwake kijiji cha Kikundi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa UDP Mkoa Dominick Ponela, Katibu huyo alikuwa akisumbuliwa na Maralia ya vipindi sambamba na vidonda ndani ya kifua.

Ponela amesema kuwa katibu Mng’oo amefariki majira ya saa 3 asubuhi wakiwa kwenye harakari za kumsafirisha kwenda hosipitali ya Rufaa Morogoro kwa matibabu.

Mwili wa marehemu upo nyumbani kwa baba yake mzazi kijiji kwa maadalizi ya mazishi ambapo mwenyekiti huyo amesema tayari amewasiliana na makao makuu ya chama hicho jijini Dara es salaam ili kushiriki mazishi hayo yaliyotarajiwa kufanyika kijijini hapo jana majira ya jioni.

Mng'oo ambae ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho Mkoani Morogoro na nchini pia aliwahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi, Mratibu elimu kata ya Tegetelo, Katibu wa utamaduni wilaya na mwenyekiti wa asasi binafsi ya Tushikamane.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu marehemu alikuwa na wake wawili akiwemo aliyefunga nae ndoa ya dini, mwingine aliyefunga ndoa Bomani sambamba na watoto nane.

No comments:

Post a Comment