Release No. 094
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 25, 2014
KIINGILIO TAIFA
STARS, MALAWI 5,000/-
Kiingilio cha chini cha mechi ya kirafiki kati ya Tanzania
(Taifa Stars) na Malawi (Flames) itakayofanyika Jumanne (Mei 27 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale
watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B
na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni ili kutoa fursa
kwa washabiki wengi zaidi kuishuhudia kwa vile itakuwa ni siku ya kazi.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager itawasili asubuhi ya siku hiyo hiyo ya mechi kutoka Tukuyu mkoani Mbeya
ambapo imepiga kambi yake chini ya Kocha Mholanzi Mart Nooij.
Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani
Young Chidmozi tayari ipo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotumiwa na timu
zote kama maandalizi ya mwisho kwa ajili mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON).
Wakati Stars kwenye mechi za AFCON itarudiana na
Zimbabwe jijini Harare, Flames nayo itakuwa ugenini N’djamena kukabili Chad.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment