TAASISI ya mifugo
kanda ya kati Taaliri inatarajia kuanza kutumia teknolojia ya viini tete
kuzalisha ng'ombe ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na
waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha utafiti wa taasisi hiyo Geminius
Tungu amesema kuwa mpango huo utatekelezwa kwa kushirikiana na tume ya sayansi
na teknolojia hapa nchini.
Tungu amesema kuwa uzalishaji wa viini tete ni teknolojia ya ng'ombe mmoja kuweza kuzalisha mayai matano hadi sita ambapo ngombe huyo, atachomwa sindano ya kukomaza mayai mengi kwa wakati mmoja na kuyarutubisha kwa mbegu za dume na kuzipandikiza kwa ngombe wengine ambao watasaidia kulea mimba na muda ukifika atazaa ndama wa kawaida.
Amesema uzalishaji huo umelenga kuchangia na kumfanya mfugaji aweze kijitosheleza kwa chakula na kuwa na maendeleo ya kiuchumi na kuongeza tija katika mifugo iliyopo hapa nchini.
Mkuu huyo amefafanua kuwa teknolojia hii ikifanikiwa aidha Tanzania itakuwa nchi ya kwanza katika uzalishaji wa namana hii na itasaidia wafugaji kuwa na ng’ombe bora.
No comments:
Post a Comment