JESHI la Polisi mkoa
wa Dodoma, limefanikiwa kukamata jumla ya wanawake 65 kwa kosa la kufanya
biashara ya ukahaba katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Akizungumza na Blog hii
mjini Dodoma kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, kamishina msaidizi
mwandamizi David Misime, amesema wanaweke 36 walikamatwa katika kipindi cha
mwaka 2013 na wanawake wengine 29 walikamatwa mwaka 2014.
Kamanda Misime
amesema kuwa wanawake hao walikamatwa katika mitaa mbalimbali ya mji wa
Dodoma,wakifanya biashara ya kuuza miili yao hasa nyakati za usiku ambapo baadhi yao walitozwa faini na wengine walifungwa vifungo vya nje.
Kamanda Misime ametoa
wito kwa wanawake wenye tabia hiyo kuacha mara moja ,huku akisisitiza kwamba
Polisi wataendelea kuwakamata.
No comments:
Post a Comment