MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Sunday, 25 May 2014

RAIS KIKWETE MGENI RASMI MAONESHO YA BIASHARA TANGA


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete anatarajiwa kufungua maonyesho ya pili ya kimataifa ya biashara mkoani Tanga.

Maonyesho hayo ambayo yameanza jana yanatarajiwa kufunguliwa Mei 26 na kumalizika Juni 3 katika viwanja vya Tangamano jijini hapa ambapo yatajumuisha nchi zaidi ya 30 kutoka Afrika na mataifa mengine.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga (TCCIA), Paul Bwoki alisema maonyesho hayo yanayolenga kuonyesha fursa za uwekezaji mkoani hapa yatafungua fursa za uwekezaji kutoka nje.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa
“Maonyesho haya ni ya siku 11, lakini tutatenga siku tatu za kujua namna baadhi ya bidhaa zinazozalishwa hapa ambapo katika siku ya kwanza tutaanza na Katani day, Tanga fresh, Tanapa, hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi,” alisema Bwoki na kuongeza.

“Wilaya za mkoa huu zimejipanga vizuri kuhakikisha zinatoa michango kwa wakati wakiwa na lengo la kuharakisha na kufanikisha maonyesho hayo kwa wakati”

Mapema leo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa alitembelea eneo la Tangamano kujionea maandalizi ya uwanja huo ambao kwa asilimia kubwa ulikuwa umekamilika.

No comments:

Post a Comment