MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Saturday 14 June 2014

WAKALA WA MIRUNGI AMPONZA KIJANA




JESHI la polisi mkoani hapa lina mshikilia kijana Kassimu  Athumani mkazi wa barabara ya 21 jijini Tanga kwa kukamatwa na mirungi yenye kilogram 100  na bunda 119 akisafirisha kutoka Tanga kwa kutumia fuso yenye  namba za usajili  T213 BSG kwenda  Dar es salaam.

Akiongea na mwanamkemakini.blogspor.com kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa3 asubuhi  eneo la Mkata wilaya ya Handeni.

Kanda Masawe amesema kijana huyo alikiri kupatiwa mirungi hiyo na mtu mmoja Tanga ili awapitishie wahisika eneo la Chalinze, Kibaha na jijini  Dar es salaam.

Aidha kamanda massawe amesema licha ya kuwa nchi za jirani zimeruhusu matumizi ya bangi lakini bado nchini jeshi hilo litaendelea kupambana na wanaojihusisha na uuzaji pamoja na matumizi hayo. Taratibu za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zinaendelea.

Katika tukio jingine mtoto mmoja ambaye ameitambulika kwa jina la Junior Salvatory (4) mkazi wa Kikunde amefariki dunia mara baada ya kugongwa na pikipiki.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda massawe amesema Salvatory amegongwa na mwendesha pikipiki namba za usajili T649BGS aina ya Sun L G Mathias  Yohana mwenye umri wa miaka 49.

Aidha amesema mototo huyo aligongwa huko kijiji cha Tonguni mnamo juni 11 majira ya saa11 za jioni.

Sambamba na hayo ametoa wito kwa wale wote watakao kamatwa na madawa ya kulevya kuwa jeshi la polisi litapambambana nao hadi hatua ya mwisho na amewataka walezi wawatoto wasiwaachie watoto wakizurura barabarani hali ambayo inaweza ikahatarisha maisha yao.

UKATILI HADI LIN!I: KICHANGA ATUPWA NDANI YA TUNDU LA CHOO

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja anaesadikiwa kuwa mkaazi wa mji wa Pongwe jijini Tanga ambaye hakuweza kutambulika mara moja amejifungua mtoto mwenye jinsia ya kike kisha muda mfupi baadae kumtupa chooni.

Tukio hilo la kinyama na la kusikitisha limetokea usiku wa Juni 12 ambapo watu wengi walikuwa makini kwenye luninga zao kufuatilia mchezo wa kwanza wa michuano ya kombe la Dunia unaoendelea nchini Brazil.
Muonekano wa Choo hicho kwa nje
 
Wakizungumza mwanamkemakini.blogspot.com wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa wamefanya jitihada za kumnusuru mtoto huyo licha ya kuwa hadi sasa mtuhumiwa hajatambulikana.

Hili ndilo tundu alimo tupwa kichanga hicho
Nae Balozi wa mtaa wa Misufini Mohamed Mbogo amekiri kupokea taarifa hizo alizozipata asubuhi ya majira ya saa 1:30 Juni 13 kutoka kwa Polisi Jamii.
Majirani wakiwa kwenye nyumba alipotupwa kichanga chooni

Mtoto huyo kwa sasa anaendelea kupata matibabu kwenye hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kumbaini aliefanya ukatili huo.

Monday 9 June 2014

MFANYABIASHARA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI TANGA

 
MFANYABISHARA mmoja mkazi wa Michungwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Ally Rajabu Makufya 72, amejiua kwa kujipiga risasi ya shingo kwa kutumia bunduki.

Marehemu ambaye pia ni mmiliki wa baa mbili wilayani Muheza amejiua June 8 majira ya saa 3; 30 asubuhi akiwa chumbani kwake akitumia bunduki yake anayoimiliki kihalali.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga amethibitisha tukio hilo.
Wakati huohuo June nane majira ya saa 8:20 mchana watu wa wawili Jofrey Daniel (20) mkazi wa kwanjeka na Musa Hamisi miaka 44 mkazi wa Mtambwe Mkoani hapa wamekamatwa wakiwa na bunduki Raifo yenye namba 2703520 iliyowahi kuripotiwa na Musa Hamisi 44 kwamba imeibiwa.

Watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamekamatwa maeneo ya Ngomeni barabra kuu ya Muheza -Tanga pia wakiwa na risasi mbili za bunduki hiyo, ganda moja la risasi, panga moja, kisukimoja na bisi bisi mbili.

MAJAMBAZI YATOKOMEA NA T.SH 1,378,600 ZA MFANYABIASHARA



WATU wanaodhaniwa kuwa majambazi wapatao nane wakiwa na silaha mbalimbali za jadi wamemvamia na kumopora fedha mfanyabiashara mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Mfanyabiashara huyo ambae ni mkazi katika kijiji cha Jasini wilayani Mkinga alitambuliwa kwa jina la Mohamed Tembo 30. Watu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga kuhusiana na Tukio hilo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Costantine Masawe amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa Tembo alivamiwa usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7:30 usiku ambapo pia walifanikiwa kutokomea na fedha taslimu sh 978,600/=.

Katika tukio jingine la June 8 mwaka huu majira ya Saa 2:30 usiku huko Pingoni Mjohoroni Pande Mkoani hapa, Sixmudi Kakurumu 62 mkazi wa Pande amevamiwa na watu wasiojulikana na kumjeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumpora sh 400,000/=.

Watu hao wapatao nane waliokuwana na silaha za jadi ikiwemo mapanga na marungu walipora pia vitu mbalimbali vya dukani ambavyo thamani yake haikuweza kufahamika mara moja

Kamanda Masawe amesema wanaendelea kufanya juhudi za kuwapata watuhumiwa hao wakati Kakurumu akiendelea kuuguza majeraha katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo.

Friday 6 June 2014

POLISI WARUKA MTEGO WA RUSHWA, YAWATIA MBARONI WASHUKIWA DAWA KULEVYA


JESHI la polisi mkoani Tanga linamshikilia kijana Said Abdalah mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Kwanjeka mjini hapa kwatuhuma za  kukamatwa na madawa yanayoyo dhaniwa kuwa  ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilogram moja.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Costantine Masawe
Mtuhumiwa huyo amekamatwa mnamo juni 4 majira ya saa nane mchana.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga, ACP Costantine Masawe akiwa ofisini kwake amesma mtuhumiwa  ambaye pia ni mfanya biashara wa Makorora mjini humu amekamatwa kupitia taarifa zilizotoka kwa raia wema.

Kamanda Masawe amesema baada ya taarifa ndipo askari walifika eneo alipokuwamtuhumiwa na kumkamata na kwamba mpaka sasa thamani ya madawa hayo haijatambulika hadia  mkemia wa serikali atakapotoa uthibitisho wa dawa hizo na uzito wake halisi.

Masawe amesema wakiwa katika harakati za kushughulikia suala hilo watu wawili Amri Mohoreja mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Donge na Hassan Mwandani mwenye miaka 24 mkazi wa Mikanjuni walitaka kuwashawishi maofisa Polisi kupokea rushwa ya shilingi 8,600,000 ili wapindishe ukweli na kumwachia mtuhumiwa.

Amesema watu hao baada ya kusikia kukamatwa kwa mwezao Said Abdala mtuhumiwa wa madawa hayo ya kulevya waliwasiliana kwa njia ya simu na maafisa wa polisi ambao waliwekeana miadi ya kukutana eneo la Harbours Club. 

Mtu aliyeathiriwa na utumiaji wa dawa vya Kulevya
Amesema ndipo Juni 4 majira ya 2;30 usiku walifanya mtego na kufanikiwa kuwatia nguvuni wakiwa na fedha hizo. 

Taratibu za kisheria zinaendelea ili watuhumiwa kufikishwa mahakamani huku akiwapongeza askari wake kwa kukataa kupokea rushwa na kuitaka jamii kuzidi kushirikiana nao kufichua wanaousika na uhuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya nchini.

Thursday 5 June 2014

WANWAKE WATAKIWA KUTOBWETEKA



WANAWAKE Mkoani Morogoro wametakiwa kutokata tamaa katika shughuli za kiuchumi ili kuondokana na utegemezi pia ombaomba kwa wanaume zao na jamii.

 Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa umojawa wanawake mkoa wa morogoro Mariam Kyamani kwenye sherehe ya miaka 10 ya kikundi cha kijamii cha Upendo women group  kilichopo kata na mtaa wa Tubuyu manispa ya Morogoro.

Kyamani ambaye pia ni diwani wa kata ya Kingolwila amesema dhana ya mwanamke kuendelea kuwa tegemezi imepitwa na wakati badala yake wanatakiwa kujishugulisha kulimngana na flsa walizonazo.

Katika risala ya kikundi hicho pamoja na mambo mengine iliomba mashirika na taasisi mbalimbali kuendelea kusaidia vikudi vya kijamii kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kinamama ya kiuchumi.

Naye katibu wa mbunge Morogoro mjini Morisi Masala aliyemwakilisha mbunge huyo aliwataka wanawake kusitahimili mikikmiki inayojitokeza katika vikundi na kuzitatua zao  ili kuimalisha vikundi hivyo. 

Amesema katika vikundi hivyo wajitahidi kuboresha elimu  kwa kuwapeleka watoto shule kwa kipato kidogo wanacho kipata.

Upendo women group kilianznzishwa mwaka 2005 kikiwa na wanachama 6 kwa lengo la kusaidiana katika shida na raha .

Kikundi hicho ambacho sasa kinawanachama 30 mpaka sasa kimeshatoa huduma mbalimbali za kijamii kwa watoto yatima na wazee wasiojiweza katika mtaa wa Tubuyu katani humo.

Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kikundi hicho martha Tanika kikundi hicho kinajiendesha kwa kutumia ada zao wenyewe na miradi mbalimbali ya  kukodisha maturubai ,zabuni za kupika chakula cha sherehe na shughuli za kupamba katika sherehe.