MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Friday 30 May 2014

TANZANIA NAFASI YAPILI MICHEZO



Tanzania imeshika nafasi ya pili kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya jana (Mei 29 mwaka huu) kuilaza Afrika Kusini mabao 2-0.

Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa SSKB jijini Gaborone ambapo kwa matokeo hayo Tanzania imetwaa medali ya fedha baada ya kushika nafasi ya pili. Nigeria ndiyo ilishika nafasi ya kwanza na kutwaa medali ya dhahabu.

Tanzania imemaliza ikiwa na pointi kumi ambapo ilishinda mechi tatu, sare moja na kupoteza moja mbele ya Nigeria.

Katika mechi ya kwanza ilitoka sare ya bao 1-1, ikawafunga Botswana 2-0, Swaziland wakachapwa 3-0 na baadaye kuwafunga Afrika Kusini 2-0. Timu ya Tanzania inayofundishwa na kocha Abel Mtweve ilifungwa na Nigeria mabao 2-0. 

Wachezaji 16 waliounda kikosi hicho cha Tanzania katika michezo hiyo inayomalizika leo (Mei 30 mwaka huu) ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.

Nchi nyingine zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland wakati Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zilijitoa dakika za mwisho.

KATIBU UDP MOROGORO AFARIKI DUNIA

KATIBU wa chama cha United Democratic Party UDP mkoa wa Morogoro Ununi Mn’goo (61) amefariki dunia May 28 nyumbani kwake kijiji cha Kikundi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa UDP Mkoa Dominick Ponela, Katibu huyo alikuwa akisumbuliwa na Maralia ya vipindi sambamba na vidonda ndani ya kifua.

Ponela amesema kuwa katibu Mng’oo amefariki majira ya saa 3 asubuhi wakiwa kwenye harakari za kumsafirisha kwenda hosipitali ya Rufaa Morogoro kwa matibabu.

Mwili wa marehemu upo nyumbani kwa baba yake mzazi kijiji kwa maadalizi ya mazishi ambapo mwenyekiti huyo amesema tayari amewasiliana na makao makuu ya chama hicho jijini Dara es salaam ili kushiriki mazishi hayo yaliyotarajiwa kufanyika kijijini hapo jana majira ya jioni.

Mng'oo ambae ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho Mkoani Morogoro na nchini pia aliwahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi, Mratibu elimu kata ya Tegetelo, Katibu wa utamaduni wilaya na mwenyekiti wa asasi binafsi ya Tushikamane.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu marehemu alikuwa na wake wawili akiwemo aliyefunga nae ndoa ya dini, mwingine aliyefunga ndoa Bomani sambamba na watoto nane.

Thursday 29 May 2014

MUME AMSHITAKI MKEWE KWA KUMNYIMA NGONO


Majaji waliamua kuwa mkewe Mason hakufanya kosa lolote

Kuna kisa kimeibuka nchini Uingereza ambapo mwanamume mmoja kwa jina David Mason, mwenye umri wa miaka 30, alimshitaki mkewe Brenda kwa kumnyima haki yake ya kingono au kukataa kushiriki tendo la ndoa.

Mwanamke huyo alimfanyia mgao wa wiki moja kila mwezi wa kitendo cha ndoa mumewe kwa hofu ya kushika mimba kwa mara ya tatu.

Kwa mujibu wa jarida la mtandao la Mirror, la Uingereza, Bwana Mason, ambaye kazi yake ni fundi mitambo alishinda kesi hiyo mwaka 1980.

Lakini mkewe alikataa rufaa ambapo Mason alipoteza kesi hiyo baada ya majaji kusema kuwa mahakama isingeweza kuamua kuwa mkewe Mason alimkosea.

Habari hii ni kwa msaada wa mtandao wa BBC

VIINI TETE KUZALISHIA NG'OMBE


  

 TAASISI ya mifugo kanda ya kati Taaliri inatarajia kuanza kutumia teknolojia  ya viini tete kuzalisha ng'ombe ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari  mkuu wa kitengo cha utafiti wa taasisi hiyo Geminius Tungu amesema kuwa mpango huo utatekelezwa kwa kushirikiana na tume ya sayansi na teknolojia  hapa nchini.

Tungu amesema  kuwa  uzalishaji wa viini tete ni teknolojia ya  ng'ombe mmoja kuweza  kuzalisha  mayai  matano hadi sita ambapo  ngombe huyo, atachomwa sindano  ya kukomaza mayai  mengi kwa wakati mmoja  na kuyarutubisha  kwa mbegu za dume na kuzipandikiza  kwa  ngombe wengine ambao watasaidia kulea  mimba  na muda ukifika    atazaa ndama wa kawaida.

Amesema uzalishaji huo  umelenga  kuchangia  na kumfanya mfugaji aweze kijitosheleza kwa chakula  na kuwa  na maendeleo ya kiuchumi  na kuongeza tija katika  mifugo  iliyopo  hapa nchini.

Mkuu huyo amefafanua kuwa teknolojia hii ikifanikiwa aidha Tanzania  itakuwa nchi ya kwanza  katika uzalishaji wa namana hii na itasaidia wafugaji kuwa na ng’ombe bora.

KAMATI YASEMA HAIRIDHISHWI UTEKELEZAJI KIGAMBONI


Ester Bulaya, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Mara na Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira


 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imesema hairidhishwi na mkakati wa utekelezaji wa Mradi wa Kigamboni.

Kamati hiyo imefikia hatua hiyo toka mchakato huo uanze kumekuwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na malalamaiko ya wakazi wa eneo husika .

Kauli hiyo imetolewa leo na  mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Ester Bulaya alipokuwa akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa kusema kumekuwa na malalmiko mengi toka kwa wananchi wa eneo hilo kuwa mchakato huo wa uandaaji wa mpango kabambe wa mji mpya haukuzingatia sheria ya mipango miji namba 8 ya mwaka 2007.

Ester Amesema mbali ya kutofuatwa kwa sheria hiyo pia wananchi wa eneo hilo walikatazwa kukarabati na kufanya shughuli za kimaendeleo katika maeneo yao huku utekelezaji wa mchakato huo kuwa wa muda mrefu kiasi cha kukatisha tama.

Amesema kutokana na changamoto hizo kamati yake inaitaka Serikali kuanza mara moja kukamilisha maandalizi ya mpango kabambe na kuanza utekelezaji wa mradi.

65 MBARONI KUSHIRIKI UKAHABA

JESHI la Polisi mkoa wa Dodoma, limefanikiwa kukamata jumla ya wanawake 65 kwa kosa la kufanya biashara ya ukahaba katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.




Akizungumza na Blog hii mjini Dodoma  kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, kamishina msaidizi mwandamizi David Misime, amesema wanaweke 36 walikamatwa katika kipindi cha mwaka 2013 na wanawake wengine 29 walikamatwa mwaka 2014.



Kamanda Misime amesema kuwa wanawake hao walikamatwa katika mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma,wakifanya biashara ya kuuza miili yao hasa nyakati za usiku ambapo baadhi yao walitozwa faini na wengine walifungwa vifungo vya nje.



Kamanda Misime ametoa wito kwa wanawake wenye tabia hiyo kuacha mara moja ,huku akisisitiza kwamba Polisi wataendelea kuwakamata.

Wednesday 28 May 2014

HABARI ZA TANGA MAY 28, 2014

 ·    
Ramani ya Mkoa wa Tanga
 

    WAFANYA biashara wa mazoa ya nafaka na samaki waliopo barabara ya 15 Kata ya Ngamiani Kusini mijni hapa, wameiomba Halmashauri ya jiji la Tanga kusimamia usafi wa mifereji iliyopo kandokando ya barabara hiyo ambayo  imekuwa chanzo kikuu cha kuwepo kwa magonjwa ya milipuko pamoja mazalia ya mbu  hususani kipindi cha mvua.
Wakizungumza na Redio huruma ya Mkoani Tanga kwa nyakati  tofauti  Akida Ramadhani na Kimaro Gilioni wamesema wao wamekerwa na hali ya uchafu uliopo ndani ya mifereji  hiyo ambayo inasababisha maji machafu kutuama jambo amablo linahatirisha  afya wakazi wa eneo hilo.
Wafanya biashara hao wameiomba Halmashuri kuchua hatua  ya kusafisha mifereji hiyo ili maji yapite kwa uraisi badala ya wafanya biashara kuhangaika wenyewe kuwatafuta vibarua na kuwalipa wenyewe kwa muda mrefu.
Akilizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa  Mtaa wa Jamhuri Kata ya Ngamiani Kusini, Shaban Choyo amesema kuwa  ni wajibu wa kila mfanya buiashara kusimamia usafi katika eneo hilo hali ambayo itasaidia  kuondokana na magonjwa ya mlipo kama Dengue na mengineyo.
Amesema yeye kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kata watahamasisha jamii zaidi  juu ya usafi huo wa mifereji  kama wanavyo fanya katika maeneo mengine ikiwemo barabarani.


 ·       KATIKA TUKIO JINGINE
   WANANCHI wametakiwa kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabrani ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara  mkoani hapa.
Akizungumza na radio huruma cha Mkoani Tanga leo katika kipindi cha tungumze asubuhi askari wa kikosi cha usalama wa barabarani PC IMANI mesema nivyema kila mwananchi atambue umuhimu wa kujua alama za vivuko wanapo kuwa barabarani. 
Amesema vivuko hivyo vya barabarani  ambavyo ni punda milia, vivuko vinavyoongozwa na taa za barabarani  na  vivuko vinavyoongozwa na askari wa polisi endapo vitafuatwa kwa usahihi kwa asilimia kubwa vinaweza kuondoa ajali za barabarani.
Sanjari na hayo ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwapa taarifa zinazo husu uvunjifu wa sheria  za barabarani.