MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Friday 26 May 2017

HABARI MSOMAJI WANGU

Kwa muda mrefu umekosa machapisho ya blog hii kutonana na kukosa muda hasa kipindi cha miaka miwili niliyo kuwa masomoni kipekee nikuombe radhi kwa usumbufu wowote ulioupata pia nikuahidi kuwa hivi karibuni utaanza kupokea machapisho katika ukurasa huu kuhusu habari na mengine mengi. Asante.

Friday 30 January 2015

RAIS MUGABE MWENYEKITI MPYA AU



RAIS mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka tisini, sasa ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa muungano wa Afrika-AU.

Wajumbe walimteuwa Mugabe kwa kauli moja katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Ababa-Ethiopia.

Uteuzi wa Mugabe kuongoza muungano huo mkubwa ulio na wanachama zaidi ya arubaini, unaelezwa kuuingiza doa ndani ya AU, kwani Mugabe hana uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kukaa uongozini tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru mnamo mwaka wa 80.

Miongoni mwa masuala  katika ajenda ni vita dhidi ya waasi  nchini Nigeria wa kundi la Boko Haram.

UELEWA MDOGO WA WAZAZI KIKWAZO CHA ELIMU BORA KOROGWE



NA EVELYN BALOZI, KOROGWE
UELEWA mdogo kwa baadhi ya wazazi kuhusu umuhimu wa elimu umeelezwa kuwa janga la kukwamisha jitihada za serikali nchini kuwapatia elimu bora wanachi wake.

Afisa taaluma wa Korogwe Mji Elius Mavoa aliiarifu Jambo Leo juzi katika mahojiano maalumu juu ya hali ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya hiyo yenye zaidi ya Shule za Msingi 133 na Shule za Sekondari 25 ambapo shule za Serikali 24 na jumuiya ya wazazi 1.

Inaarifiwa Mkurugenzi wa Korogwe Mji, Lewis Kalinjuna katika baraza la madiwani mwanzoni mwa juma aliagiza madiwani wa kata zote kuwaelimisha wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wazingatie masomo ili kujenga Taifa lenye wataalamu.

Na katika kuhakikisha hilo Mavoa alisema halmashauri hiyo imemeba jukumu la kuwasomesha zaidi ya wanafunzi 220 wa Sekondari na Msingi wanao ishi kwenye mazingira magumu.

Kati ya wanafunzi hao wanaosomeshwa, wa sekondari ni 120 na wa shule za msingi ni zaidi ya 100.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Anjelus Bendera akifafanua zaidi alisema hatua hiyo imekuja baada ya Halmashauri kugugundua uwezo mdogo wa familia huchangia ongezeko la utoro kwa wanafunzi katika shule mbalimbali.

Alisema Halmashauri hiyo imeandaa mfuko maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao kupitia kitengo cha ukimwi na daftari la kuandikisha watoto wanao ishi kwenye mazingira magumu na hatarishi.