MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Thursday, 29 January 2015

WANASHERIA WATAKIWA KUTUNGA SHERIA NDOGO VIJIJINI



BAADA ya kubainika sheria ndogo za vijiji ‘by law’ kushindwa kuwawajibisha wanaokiuka taratibu wanasheria wa halmashauri za wilaya wametakiwa kushirikiana na serikali kutengeneza na kuboresha sheria zilizopo.

Hayo yamebainishwa na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya ufuatiliaji na uwajibikaji wa jamii kwenye sekta ya afya kwa washiriki 90 iliyojumuisha viongozi wa vijiji, kata, madiwani na wananchi wa kawaida.

Semina hiyo iliyoanza juzi inaendeshwa na shirika la Hale Development Organization HADEO.

Walisema hali hiyo imejitokeza baada ya wanasheria wa halmashauri kutokuwa tayari kufika waliko wananchi hao na kushindwa kushirikiana nao katika kutengeneza sheria zilizopo ama kuziboresha kwa manufaa ya jamii.

Awali Diwani wa kata ya Magoma Hadija Mshahara alisema iwapo watendaji watasimamia sheria kikamilifu hali ya unyonge itaweza kuwaondokea.

Kauli hiyo ya diwani huyo ilichangiwa na watendaji na wananchi wakielezea mapungufu ya kisheria yaliyopo hivi sasa wakisema zimeshindwa kufanya kazi katika eneo la Mahakama ambapo mwezeshaji wa semiha hiyo aliwakumbusha kwamba bado hilo liko kwenye uwezo wao na halmashauri.

Katika semina hiyo ya mafunzo iliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu TTC wilayani Korogwe wafadhili wa mafunzo hayo walikuwa ni shirika la The Foundation for civil society ambapo shughuli ya mafunzo iliendeshwa na shirika la Hale Development Organization HADEO la wilayani Korogwe.

Tuesday, 27 January 2015

MAGAIDI YA ALQAEDA WAWAPORA SMG POLISI


Na Mashaka Mhando,Tanga
MAJAMBAZI yanayohisiwa kuwa yamo kwenye mtandao wa Alqueda pamoja na kundi la Alshababu, imewajeruhi askari polisi na kuwapora bunduki mbili aina ya Sub-Machine Gun (SMG) zilizokuwa na risasi 60.

Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jana na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Tanga, Juma Ndaki, limetokea katikati ya mitaa ya barabara ya 4 na 5 Jijini Tanga,  nyumbani kwa Jamali Twalib mwenye biashara ya kuuza chips Jijini hapa.

Polisi hao walioporwa bunduki hizo ni mwenye namba H 507 Konstebo Mwalimu na mwenzake G 369 Konstebo Mansur ambaye amelazwa katika hospitali ya Bombo baada ya kuchomwa kisu sehemu mgongoni na shingoni wakati wa uporaji huo na hali yake bado tete katika hospitali hiyo.

Mmoja ya mashuhuda wa tukio hilo, kijana muuza Chips Jeirus Chimya, alilieleza Majira kuwa tukio hilo lilitokea majira ya 5:45 usiku wakati askari hao waliokuwa na kawaida ya kula hapo wanapokuwa doria usiku, walifika wakaagiza chakula hicho.

"Kawaida askari hawa huwa wanafika wakiwa wanne na pikipiki zao na kula chakula hapa kila siku, sasa jana walifika wawili wakasema wenzao wamewaacha kituo cha basi cha Ratco watakuja wawawekee nao chakula chao, tukawaandalia kama kawaida," alisema Chimya.

Alisema baada ya kuwaandalia chakula kile ghafla waliwaona watu wanne wakiwafuata huku mmoja akiwa amebaki kwenye kona ya barabara ya 5 kutazama watu huku akiwa na pikipiki mbili ambazo walifika nazo kwenye tukuio hilo.

Chimya alisema askari wale walikuwa pembeni ng'ambo ya barabara kwenye duka moja linalouza nguo, wakikaa peke yao ndipo mmoja wa jambazi huyo alikuwa amevaa suruali wanayovaa askari wa Kutuliza ghasia FFU na kumvamia Mansur ambaye kwa wakati huo alikuwa akinywa soda.

"Yule jamba
zi aliyeonekana kama askari polisi alipoishika ile bunduki ya Mansur ambaye alitaharuki na jambazi kutoa kisu kwa lengo la kukata mkanda wa bunduki ili aondoke nayo akamchoma kisu cha shingo, lakini askari akawa mbishi akachomwa kisu kingine cha mgongoni akaiachia bunduki," alisema muuza chips huyo.

Aliendelea kueleza kwamba majambazi wengine wawili walimshika Mwalimu naye na kumpora bunduki yake na baada ya kuleta ubishi walimpiga na kisha kuangukia kwenye mtaro na kuichukua bunduki ile kirahisi na kukimbia katika eneo hilo.

"Kukweli watu tulioshuhudia tulipigwa na bumbuwazi tukizani ni utani baina ya askari kwa askari kutokana na namna walivyokuwa wamevalia watu wale kwani baada ya kupora bunduki hizo mmoja wa majambazi alishindwa kukimbia baada ya kupoteza funguo ya pikipiki.


Alisema baada ya muda askari wengine wawili waliokuwa wamewawekea chakula walifika katika eneo hilo huku majambazi wale wakiwa tayari wameondoka lakini wakafanikiwa kumkamata jambazi mmoja ambaye alikuwa akishindwa kuwasha pikpiki kutokana na kupoteza funguo.

Akizungumza ofisi kwake tukio hilo, kaimu kamanda wa polisi JUma Ndaki, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba mmoja wa majambazi waliomkamata na kumpekua nyumbani kwake walimkuta na CD zipatazo 13 zikiwa na mafunzo ya Alqueda na Alshababu.

"Ni kweli askari wetu wamenyany'anywa bunduki zikiwa na risasi 60 na mmoja wao tumemkamata na tulipompekua alikuwa na CD zenye kuonyesha mafunzo ya Alqueda bila shaka ni washirika wa kundi hilo na hivi sasa tunafanya mipango tumsafishe Jijini Dar es salaam kwa hatua zaidi za kiuchunguzi," alisema Ndaki.
Ndaki pia alisema walimkamata mmoja wa mke wa jambazi aliyemtaja kwa jina moja la Asha ambaye aliwahi kukamatwa kisha kuachiwa kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa Alqueda na kwamba kwa sasa mumewe ni mmoja kati ya waporaji wa bunduki hizo.

Friday, 9 January 2015

UELEWA MDOGO BAADHI YA WAJUMBE SERIKALI ZA MITAA WAWAKWAMISHA WENGINE KULA KIAPO


HAFLA ya kuapishwa wenyeviti wateule wa serikali za mitaa wa Halmashauri ya jijini Tanga, imefanyika leo na kukamilika kwa kiwango kikubwa kwenye Ukumbi wa Shule ya ufudi Tanga, iliyopo kata ya Mzingani.
 
Hata hivyo uelewa mdogo miongoni mwa wajumbe hao wa serikali za mitaa, waliopatikana katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni umezua changamoto wakati wa zoezi hilo la kula kiapo hivyo italazimu kurudiwa kwa baadhi yao.
 
Akitangaza utaratibu wa kiapo Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Tanga Aziza Lutalla alisisitiza kuwa kiapo ni kifungo ambacho hakitakiwi kiwe kimefutwafutwa iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya, kauli hiyo ilizua minong’ono kwa baadhi yao hadi pale  alipotangaza kwamba kwa waliokosea kujaza fomu zao za kiapo itawalazimu kurudia kuzijaza upya kisha zitawekwa sahihi nayeye kwa utaratibu utakaopangwa.
 
“Kiapo ni ushahidi wa kukubaliana na masharti ya utumishi wa Umaa katika nafasi yako na kukiuka ni kosa la jinai na kuna adhabu yake kwa mujibu wa sheria za nchi... haitakiwi kiwe kimefutwafutwa, kwahiyo kama kuna mjumbe aliyefanya hivyo awasiliane na mratibu wa zoezi upewe fomu nyingine,” aliwasisitizia viongozi hao
 
Baada ya zoezi la Kuapishwa kwa Wenyeviti 181, wajumbe mchanganyiko 543 na wajumbe 362 wa viti maalumu, Mstaiki Meya wa Jiji la Tanga, Omari Guledi aliwasisitizia viongozi hao kuachana na itikadi za vyama vyao lakini wawe wamoja kwa kufanya vikao kwa mujibu wa taratbu kwa maslahi ya nchi.
 
Nao wajumbe hao walizungumza na Mwanamke Makini walibainishwa kuwa licha ya zoezi hilo kukamilika lakini lilikuwa na dosari ambazo hazina budi kufanyiwa kazi kwa wakati mwengine kwavile sasa limeshapita salama.
 
“Sina hakika kama wajumbe wote wanajua kusoma na kuandika, kama ulifuatilia kwa makini mwandishi wengine hawakuwa wakijaza wala kusema yale maneno ya kuapa, sasa kwasababu tuliapishwa jumla angalau imewabeba," alisema Hussein Abasi  mwenyekiti mtaa wa New Hotel kata ya central

Wednesday, 7 January 2015

UGANDA KUUNGANA NA UN VITA DHIDI YA FDLR



UMOJA wa Mataifa umesema Rais Joseph Kabila ameahidi kuwa jeshi lake litaungana na la UN katika operesheni dhidi ya waasi wa FDLR.

kikosi cha wanajeshi elfu 20 wa umoja huo watashirikiana na wale wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika kampeni zilizopangwa kuanza karibuni dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda.

Wanamgambo wa Kihutu, wanaojulikana kama FDLR, wamekuwa wakilitumia eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama kambi yao ya kufanya mnashambulizi dhidi ya serikali ya nchi jirani ya Rwanda.

Waasi hao wameshindwa kufikia muda wa mwisho wa kimataifa uliowekwa wiki hii wa kuweka silaha chini na kuondoka katika eneo hilo.

WAWIILI MBARONI MAUAJI YA WANAHABARI UFARANSA



POLISI wa Ufaransa wametoa majina na picha ya washukiwa wawili waliohusika na shambulio katika ofisi za jarida la vibonzo nchini humo.

Polisi wamemtaja Said Kouachi na kaka yake Cherif wanaweza kuwa watu hatari na wenye silaha.

Cherif Kouachi aliwahi pia na kuhusika na kupeleka wapiganaji wenye msimamo mkali wa kidini nchini Iraq.

Vyombo vya Habari vya Ufaransa vimesema mtu wa tatu ambaye amegunduliwa pia kama ni mshukiwa Hamyd Mourad mwenye umri wa miaka 18 alijisalimisha polisi baada ya kuona jila lake katika mitandao ya kijamii.

Baadhi ya rafiki zake walisema katika mitandao hiyo kwamba alikuwa shule wakati shambulio hilo katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo likitokea, ambako watu 12 waliuawa.

Uchunguzi mkali bado unaendelea kuwasaka watu hao wenye silaha.
Awali jarida hilo lilipandisha hasira kwa waislamu baada ya kuchapisha kibonzo walichodai kuwa ni Mtume Muhamad SAW.

Jana polisi nchini Ufaransa walisema kuwa wanaume waliokuwa wamejifunika nyuso wamewaua takriban watu 12 kwenye ofisi za gazeti moja la vibonzo la Charlie Hebdo.

Watu wengine watano wameripotiwa kujeruhiwa vibaya.Gazeti hilo lililo mjini Paris limekuwa likilengwa na wanamgambo wa kiislamu siku za nyuma.

Tukio hilo lilitokea mapema asubuhi wakati watu waliokuwa na silaha walipoingia katika ofisi za gazeti hilo na kuanza kufyatua risasi na kisha wakatoroka wakitumia gari.

Rais wa ufaransa Francois Hollande amelaani shambulizi hilo akisema kuwa nchi hiyo imepatwa na mshangao mkubwa.

Inaarifiwa washambulizi walisikika kwa sauti ya juu wakisema ''tumelipiza kisasi kw aniaba ya Mtume Muhammad.'

Rais Francois Hollande alisema hapana shaka kwamba shambulizi hilo ni la kigaidi

Waandishi wanne wa jarida hilo la vibonzo, akiwemo mhariri mkuu Stephane Charbonnier walikuwa miongoni mwa waliouawa pamoja na maafisa wengine wawili.

Vyombo vya habari vimewataja wachoraji wengine watatu waliouawa wakiwemo, Cabu, Tignous na Wolinski. Duru zinasema shambulizi hilo lilifanyika wakati wa mkutano wa kila mwezi wa uhariri wa jarida hilo.

WANNE WAUWAWA PONGWE KWA WIZI WA NG'OMBE



WATU wanne wameuawa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa Silaha za jadi baada ya kuwatuhumu kuiba Ng'ombe mmoja mwenye thamani ya shilingi laki saba.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Tanga Frasser Kashai amesema limetokea january 5 mwaka huu majira ya saa 20:00 usiku katika  kijiji cha Maranzara Tarafa ya Pongwe Wilayani Tanga.

Kamanda Kashai  amewataja watuhumiwa hao waliouawa kuwa ni Mwenshehe Abasi(29) na Edwin Kamugisha (25) wakazi wa  Pongwe Jamse Erick (22)mkazi wa Kange na Juma Bakari ambaye hajatambulika umri wala makazi .

imedaiwa kuwa baada ya ng'ombe huyo kuibiwa wananchi walifuatilia nyao zao na kuwakuta  watuhumiwa hao wanne wakimfunga ng'mbe huyo kwenye mti  ndipo wananchi hao walopoanza kuwashambulia hadi kuwauwa.

kufuatia mauaji hayo Jeshi  la Polisi limefanya Msako mkali na kufanikiwa kuwakamata  watuhumiwa watano wanaohusishwa na mauaji hayo ambao ni Abdi Mohamedi (29)  Kombo Mrami (23) Maendo Juma (20), Hakimu Omari (53) na Issa Bakari (53) na watuhumiwa wote watano ni wadigo wakazi wa Maranzara.

Miili ya marehemu watatu wamekabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi baada ya uchunguzi wa daktari na mwili mwingine bado umehifadhiwa katika hospital ya Mkoa Bombo ikisubiri utambuzi kutoka kwa ndugu watakao jitokeza.