![]() |
WAUMINI WA MADHEHEBU YA ROMAN KATHOLIKI [RC] JIMBO LA DODOMA WAKIWA KATIKA IBADA. |
BABA MTAKATIFU Fransisco amelifanya jimbo katoliki Dodoma
kuwa Jimbo Kuu la sita nchini Tanzania.
Hata hivyo mara baada ya kulipandisha hadhi Jimbo katoliki
Dodoma kuwa Jimbo Kuu amemteua Askofu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Katoliki mbulu
kuwa askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma.
Kwa hivi sasa jimbo kuu teule litakuwa linasimamia majimbo
ya Kondoa na Singida.
Askofu Mkuu Mteule Beatus Kinyaiya alizaliwa tarehe
9 may 1957 Shimbwe Jimbo katoliki Moshi ambapo tarehe 5 Juni 1988 alipokelewa
kwenye shirika la wakapuchini na tarehe 25 Juni 1989 alipewa daraja
Takatifu la Upadre.
Aidha Askofu mkuu mteule mnamo mwaka 2006 aliteuliwa kuwa askofu
wa Jimbo katoliki Mbulu na alisimikwa tarehe 2 Julai akishika
nafasi ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Mwanza Yuda Tahadeus Ruwaichi aliyekuwa
askofu wa Jimbo hilo kwa kipindi hicho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Jimbo
katoliki Dodoma imesema kuwa maandalizi ya kusimikwa kwa askofu
Mkuu mteule yanatarajiwa kuanza mapema.
No comments:
Post a Comment